Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba katikati ya bato la Arsenal, PSG

BATO Pict

BUDAPEST, HUNGARY: PSG ndiyo mabingwa wa Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo, wakichukua mara hii mbele ya mabingwa wa Ligi Kuu England, Arsenal.

Lakini, Arsenal, kiuhalisia ndio waliostahili ubingwa huo iwapo karata zao wangezichanga ipasavyo katika mchezo huo ambao waliukamata vilivyo katika dakika za mwanzo na kupata bao la kuongoza la Kai Havertz alilolifunga katika mazingira magumu. Hata hivyo, mwisho waliocheka walikuwa PSG.

BAT 01

UCHAMBUZI WA KITAKWIMU WA MCHEZO

PSG sasa wamefunga mabao 45 katika Ligi ya Mabingwa msimu huu wakifikia rekodi iliyowekwa na Barcelona 1999-2000 ya kufunga mabao mengi zaidi katika kampeni moja ya mashindano hayo.

Hata hivyo, Arsenal waliruhusu mabao saba tu katika mashindano yote msimu huu, na walionyesha tena nidhamu kubwa ya kiuchezaji chini ya kocha Mikel Arteta.

Pengine ndiyo sababu haikushangaza kuona fainali hii ya Ligi ya Mabingwa iliamuliwa kwa mikwaju ya penalti kwa mara ya kwanza tangu 2016.

Licha ya uimara huo wa Arsenal, PSG walikuwa na ubora kushambulia. Katika dakika 120 za mchezo, PSG walipiga mashuti 21 na kutengeneza kiwango kikubwa zaidi cha mabao yanayotarajiwa ikiwa ni mara mbili zaidi ya wapinzani wao, wakati Arsenal walipiga mashuti saba pekee, moja tu likilenga lango.

BAT 02

Shuti hilo moja ndilo lililozaa bao la Kai Havertz ambalo lilimfanya Mjerumani huyo sasa kuwa mchezaji wa tatu katika historia kufunga mabao kwenye fainali za Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu mbili tofauti (Chelsea na Arsenal), baada ya Cristiano Ronaldo (Manchester United na Real Madrid) pamoja na Mario Mandzukic (Juventus na Bayern Munich). Hata hivyo, safari hii alijikuta upande uliopoteza.

Hii ilikuwa fainali ya 13 katika historia ya Kombe la Ulaya na Ligi ya Mabingwa kwa pamoja kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti na timu kutoka England zimehusika katika fainali tano kati ya sita za mwisho zilizofikia hatua hiyo.

Baada ya kumaliza ukame wa miaka 22 bila ubingwa wa Ligi Kuu England, Arsenal bado wanaendelea kusubiri taji kubwa zaidi la soka la klabu Ulaya.

Kwa upande mwingine, Kocha wa PSG, Luis Enrique ameendeleza rekodi yake ya kipekee kwa kushinda fainali zote tatu za Ligi ya Mabingwa ambazo amehusika kama kocha.

Kocha huyo aliwatumia wachezaji walewale 10 uwanjani aliowatumia PSG walipoifunga Inter Milan mwaka mmoja uliopita, na hivyo kuisaidia PSG kuwa timu ya kwanza kushinda ubingwa wa ligi ya nyumbani na Ligi ya Mabingwa katika misimu miwili mfululizo, na wamekuwa timu ya pili katika karne hii kutwaa Ligi ya Mabingwa katika misimu miwili mfululizo (2025 na 2026), baada ya Real Madrid kufanya hivyo 2016 na 2018.

BAT 03

Pia ni timu ya kwanza kutoka Ufaransa kushinda Kombe la Ulaya au Ligi ya Mabingwa katika misimu miwili mfululizo.

Arsenal imekuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligi ya Mabingwa kushindwa kulenga lango katika mikwaju miwili ya penalti kwenye fainali ikiwa ni zile za Eberechi Eze na Gabriel Magalhaes, huku timu hiyo ikiwa na wastani wa umiliki wa mpira wa asilimia 24.7, kiwango cha chini kabisa kuwahi kurekodiwa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu 2003-04.

Huo pia ulikuwa umiliki wa mpira wa chini zaidi kwa Arsenal katika mechi yoyote chini ya kocha Mikel Arteta na walicheza wakiwa na wachezaji 11 uwanjani kwa muda wote wa mchezo.

Kwa jumla, takwimu zinaonyesha licha ya Arsenal kuonyesha nidhamu kubwa ya kujilinda, PSG walikuwa na ubora zaidi katika kutengeneza nafasi za kufunga.