Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri nyuma ya viatu vya mastaa NBA

NBA Pict

Muktasari:

  • NBA ndiyo mashindano yenye hadhi ya juu zaidi katika michezo duniani yakiwa na mzunguko wa pesa wa wastani wa Dola 10.02 bilioni za Marekani kwa mwaka kutokana udhamini, malipo kwa wachezaji na mikataba mipya inayoingiwa na klabu, wachezaji na taasisi za biashara na kadhalika.

WASHINGTON, MAREKANI: UNAZIJUA sneaker? Hivi ni viatu vya wachezaji wa NBA. Ndiyo,wachezaji wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), mara nyingi huvaa viatu vya hali na hadhi ya juu (high-top sneakers) kwenye matangazo yao ya kibiashara, lakini ndivyo wanavyotumia kuchezea katika mechi.

NBA ndiyo mashindano yenye hadhi ya juu zaidi katika michezo duniani yakiwa na mzunguko wa pesa wa wastani wa Dola 10.02 bilioni za Marekani kwa mwaka kutokana udhamini, malipo kwa wachezaji na mikataba mipya inayoingiwa na klabu, wachezaji na taasisi za biashara na kadhalika.

Hata hivyo, unapozungumzia viatu vinavyovyaliwa na mastaa wa NBA unazungumzia biashara nyingine kabisa katika tasnia ya michezo duniani, kwani mastaa wanaoshiriki mashindano hayo takriban 510 kwa timu 30 za ukanda wa Mashariki na Maghariki, ni vya kipekee na thamani yake ni kubwa. Mathalan, kiatu cha bei ya chini unachokiona kimevaliwa na mchezaji wa NBA kinaanzia Dola 700 za Marekani.

NB 01

VIJUE ZAIDI

Viatu hivyo vinavyotengenezwa na kampuni za vifaa vya michezo hutengenezwa ili kutoa msaada wa ziada kwenye vifundo vya miguu unaowezesha ustahimilivu kwa mchezaji anapokuwa uwanjani katika kila hali ikiwamo kuruka juu, chini, anapoteleza na pia anapokanyaga sakafu ya uwanja.

Miundo ya ndani ya unyayo inavutia na huwafanya wachezaji kuna na ulinzi wa ziada wakati wa michezo na pia kuwa rahisi kwao kufanya lolote uwanjani. Kila unapokaribia msimu wa mashindano hayo matangazo na kampeni za kibiashara na chapa za viatu mara nyingi huonyesha miundo ya hali ya juu inayotengenezwa kwa teknolojia bunifu za kipekee.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba wachezaji wengi wa NBA pia huvaa viatu vya chini (low-top sneakers) kwa sababu ya uzito kuwa mwepesi na muundo unaonyumbulika. Uamuzi wa kuvaa viatu vya juu au vya chini hutegemea na mapenzi binafsi ya mchezaji na mtindo wa uchezaji.

Mathalan, mchezaji wa ulinzi anapenda zaidi kutumia viatu vinavyomwezesha kuhimili purukushani au minyukano anayokutana nayo pale anapokabiliana na washambuliaji kwa kuwa wanapolisakama lango huwa katika kasi na pia kuruka ili kutupia mpira wavuni ni jambo la kawaida kwao.

Kwa nini wachezaji wa kikapu hupaka mafuta chini ya viatu vyao mara kwa mara wakati wa mechi? Mara nyingi mastaa hao hupaka au kufuta chini ya viatu vyao kwa kutumia mafuta flani hivi laini wakati wa mechi ili kuboresha mshiko (traction).

Inadaiwa kwamba vumbi, uchafu na unyevu vinaweza kukusanyika kwenye nyayo za viatu, jambo ambalo hupunguza uwezo wa kiatu kikanyagapo kushika vyema sakafuni na kufanya iwe vigumu kufanya mizunguko ya ghafla, kusimama na kuanza tena haraka uwanjani.

NB 05

Kwa kupaka au kufuta nyayo za viatu, wachezaji huondoa vitu hivyo na kurejesha mshiko wanaohitaji ili kucheza kwa ufanisi. Pia, wachezaji wengi huwa na imani au desturi zinazohusiana na kitendo hicho, lakini sababu kuu ni kuvifanya kushika vyema katika sakafu ya uwanja.

Vilevile viatu vinaweza kuteleza kutokana na unyevu au vumbi. Kwa hiyo wanapofuta sehemu ya chini ya viatu vyao, wanarudisha mshiko (traction) ili waweze kucheza vizuri zaidi na kupunguza hatari ya majeraha.

NB 02

Pia, mshiko huo ni muhimu kwa ajili ya kusimama na kuanza kwa haraka kucheza, kukimbia au kurusha mpira bila kutetereka na pia kuzunguka ghafla na kubadili mwelekeo. Hizo ni miongoni mwa mbinu kubwa za kimwili zinazohitajika ili kucheza mpira wa kikapu kwa ufanisi bila kujali ukubwa au nafasi ya mchezaji.

Unapoangalia mechi za NBA, je huwa unamuona mtoto au mtu mzima anayekimbia na kifaa chenye mto chini kufutia sakafu? Ufutaji wa sakafu (uwanja) ni jambo muhimu kwa ajili ya kuwezesha viatu kutoshika vumbi kwa urahisi. Mtu huyo hufuta jasho sakafuni linalodondoka kwa wachezaji, lakini pia anafuta vumbi. Sakafu za mpira wa kikapu hukusanya vumbi, na vumbi hilo likikaa chini ya viatu husababisha utelezi.

Njia ya moja kwa moja ya kukabiliana na hali hiyo ni kufutwa kwa sakafu na vifaa maalumu na pia mchezaji kutumia mafuta flani kwa ajili ya kusafisha sehemu ya chini ya kiatu (sole) ili kukifanya kiatu kiwe safi. Baada ya kufutwa, viatu  hutengeneza ule mlio wa “squeak” unaoashiria kuwa mshiko umerudi yaani vinashika vyema sakafuni.

NB 03

Wachezaji wa kikapu huondoa insole (vipande vya ndani vya viatu) kabla ya kuwapa watu wengine kwa sababu mbalimbali.  Mara nyingine ni kwa sababu wanavitumia binafsi kwa viatu tofauti au huwa zimeundwa kwa maumbile yao binafsi.

Hata hivyo, unaposoma hapa elewa kwamba ingawa viatu vinavyotumiwa na mastaa wa kikapu vinaweza kutumika kukimbilia umbali mfupi, havifai kutumiwa kukimbilia umbali mrefu kwa sababu ya uzito na muundo ambao hautarajiwi kwa mizunguko ya kurudia-rudia ya kukimbia. Ndiyo maana wao huvitumia kukimbia kwa mita zisizodi 10 au 12 uwanjani.

Lakini umeshwahi kuona wachezaji wa kikapu wakigusa chini ya viatu vyao? Nyota hao hufanya hivyo ili kujua kama kuna mshiko bora kwenye viatu vyao yaani kujua kama yale mafuta ya kuvifanya vikanyagapo vishike vyema sakafuni yangalipo. Wakati mwingine sakafu huwa na vumbi au unyevu, hivyo wanapobaini vinginevyo chini ya viatu huboresha kwa kuvipaka upya mafuta au hayo au kuvivua na kuvaa vingine ambavyo huwa nayo.

Katika michezo mingi ya kikapu ya vyuo (NCAA) na karibu kila mchezo wa shule za sekondari nchini Marekani hutumia taulo zenye unyevunyevu zinazowekwa karibu na mahali wanapokuwa makocha wa timu wakati wa robo ya kwanza ya mechi. Hiyo ni sababu ileile inayofanya ‘waoshaji’ kusafisha uwanja wote wa futi 94 dakika 30 kabla ya kila mchezo.

NB 04

Kwa nini wachezaji wa kikapu wanapendelea viatu vinavyotoa sauti ya mlio (squeak) sakafuni? Ukweli ni kwamba hawapendelei tu mlio huo, bali wanapenda kile mlio huo unamaanisha. Kwa kawaida, viatu vyenye mshiko mzuri ndivyo hutengeneza mlio huo. Ni kama vile miaka ya zamani mtu alipokuwa akivaa viatu vipya kwa mara ya kwanza shuleni - unavisikia vikitoa mlio wakati unatembea, kwa sababu bado ni vipya na vina mshiko bora sakafuni.

Wachezaji wa kikapu wanahitaji viatu vyenye mshiko wa hali ya juu ili waweze kusimama na kuanza kukimbia kwa haraka. Ndiyo maana unasikia milio hiyo sana wakati wa mechi - inamaanisha viatu vina mshiko mzuri kwenye sakafu ya uwanja.

Je, wachezaji wa mpira wa kikapu ni maarufu kwa viatu vyao? Ndiyo, wachezaji wengi wa mpira wa kikapu hulipwa ili kuvaa viatu maalumu. Wanapolipwa kufanya hivyo, ni kwa sababu mamilioni ya watu huwaangalia na hupenda kununua viatu wanavyovaa wachezaji wao wanaowapenda. Kwa hiyo, ndiyo maana wachezaji wa mpira wa kikapu ni maarufu kwa viatu vyao.


Kwa nini viatu vya mpira wa kikapu hutoa milio ya “squeak”?

Soli za viatu vya mpira wa kikapu hutengenezwa kwa mpira laini na unaobebeka kirahisi. Huwa na mistari midogo ambayo husaidia kushika sakafuni vizuri, lakini pia kumruhusu mchezaji kubadilika mwelekeo kwa haraka. Tofauti na viatu vya michezo mingine, viatu vya kikapu pia hutengenezwa kuhimili kuruka mara kwa mara, hivyo vinahitaji kuwa na unene wa kutosha, lakini pia viwe laini na mchezaji anahimili kuvitumia. Kwa nini wachezaji wengine hufuta mikono yao kwenye viatu? Wapo mastaa wa NBA ambao hufanya hivyo ikiwa ni njia ya kuondoa jasho mikononi na pia kusaidia kufuta vumbi kwenye viatu. Mikono yenye jasho inaweza kusaidia kusafisha kidogo chini ya viatu, na hivyo kuboresha mshiko.

Akizungumzia ishu ya viatu vya kuchezea, staa wa zamani wa kikapu aliyeichezea Boston Celtics, Larry Bird anasema wakati akicheza alikuwa akisafisha viatu vyake kwa mikono ili mikono ibaki kuwa mikavu, na baada ya hapo ikawa kawaida kwa wachezaji wa NBA kufanya hivyo. Hata hivyo kwa sasa wengine wanasema hufanya hivyo kwa ajili ya kukausha mikono tu, huku pia kukiwa na wale wanaodai kwamba hurudia-rudia kufanya hivyo kama njia ya kuondoa msongo wa mawazo au wasiwasi mchezoni, ilhali wapo wanaosema huondoa chembechembe za mchanga au vumbi vinavyoweza kusababisha mchezaji kuteleza.

Lakini, Kocha Mkuu wa New York Knicks, Tom Thibodeau anasema wachezaji wa kikapu hufanya hivyo ili kuepuka hali ya viatu kuteleza.

“(Enzi zangu) nikiwa uwanjani mara nyingi nilikumbwa na matatizo ya kukosa mshiko mzuri (sakafuni), hasa viatu vinapokuwa na unyevu. Nilishawahi kuanguka wakati nikijaribu kuzuia mpinzani na kuumia kifundo cha mguu. Tangu siku hiyo nilikuwa nahakikisha viatu vyangu havina unyevu na viko tayari kwa mchezo,” anasema Thibodeau.