Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakali wa asisti msimu mmoja Ligi Kuu England

ASIST Pict

Muktasari:

  • Wafungaji wa mabao hupata sifa nyingi, lakini katika miaka ya karibuni inaonekana kana kwamba wale wanaowapa pasi za mwisho wameanza kuthaminiwa zaidi na zaidi.

LONDON, ENGLAND: KUTOKANA na Bruno Fernandes kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuvunja rekodi ya pasi za mwisho (asisti) nyingi zaidi katika msimu mmoja wa Ligi Kuu England, hawa ndio bado anapaswa kuwazidi ili awe kinara.

Wafungaji wa mabao hupata sifa nyingi, lakini katika miaka ya karibuni inaonekana kana kwamba wale wanaowapa pasi za mwisho wameanza kuthaminiwa zaidi na zaidi.

Ndiyo, wakati mwingine asisti inaweza kuwa rahisi kama kuupiga mpira umbali wa mita moja kwa mchezaji aliyepo katikati ya uwanja ambaye anawapita wachezaji watano na kufunga kwa shuti la mbali, lakini mara nyingi ni pasi iliyopangwa vizuri inayompa mchezaji nafasi ya dhahabu ya kufunga bao.

Tayari kuna mastaa wale waliotoa asisti nyingi zaidi kwa ujumla katika historia ya Ligi Kuu England, lakini pia wapo wa kuangaliwa waliofanya hivyo zaidi katika msimu mmoja. Thierry Henry na Kevin De Bruyne wanashikilia rekodi hiyo wakiwa na asisti 20, lakini ilionekana kuwa hatarini  msimu wa 2024-25. Zikiwa zimebaki mechi takriban tano, Mohamed Salah amefikisha asisti 18 kwa Liverpool, lakini Mmisri huyo alishindwa kuongeza nyingine zaidi na hatimaye akabaki nyuma ya De Bruyne na Henry. Lakini, msimu unapoelekea hatua za mwisho , Bruno Fernandes akiwa na asisti 18 hadi wiki hii yupo katika nafasi ya kushindania rekodi hiyo.

ASIS 01

20 – Kevin De Bruyne (2019-20)

Katika msimu wa 2019-20, Kevin De Bruyne alimaliza kusubiri kwa miaka 17 kwa mtu yeyote kufikia idadi ya ajabu ya asisti 20 ya Thierry Henry 2002-03 Ligi Kuu England. De Bruyne alifikia idadi hiyo katika michezo 35, miwili pungufu kuliko Henry, na aliweka angalau asisti saba zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote katika ligi msimu huo, mbele ya Trent Alexander-Arnold wa Liverpool (13) aliyekuwa nafasi ya pili.

Kiungo huyo wa zamani wa Manchester City alikuwa katika kiwango cha juu msimu huo, licha ya ukweli kwamba kikosi cha Pep Guardiola kilishindwa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England kikimaliza pointi 18 nyuma ya mabingwa, Liverpool.

De Bruyne ana misimu minne kati ya 11 bora zaidi katika historia ya Ligi Kuu England kwa asisti, pia akipata 18 katika msimu wa 2016-17, na 16 ule wa 2017-18 na 2022-23. Anashika nafasi ya pili katika orodha ya asisti nyingi zaidi za muda wote katika mashindano hayo nyuma tu ya Ryan Giggs.

ASIS 02

20 – Thierry Henry (2002-03)

Wakati mafanikio ya jumla ya De Bruyne 2019-20 yalikuwa mazuri, akiwa na mabao 13 pamoja na asisti 20, hayakuwa makubwa kama Henry 2002-03, ambapo mshambuliaji huyo wa Ufaransa aliongeza mabao 24 pamoja na asisti 20.

Jumla ya michango yake 44 ya mabao kwa Arsenal msimu huo ni moja ya kiwango cha juu zaidi kuwahi kufikiwa na mchezaji katika msimu wa mechi 38 wa Ligi Kuu England.

Jumla ya Henry ilijumuisha mechi moja aliyotoa asisti tatu katika ushindi wa Arsenal wa mabao 4-0 dhidi ya Sunderland katika Uwanja wa Stadium of Light, Mei 2003, huku pia akitoa asisti mbili katika mechi nne nyingine.

ASIS 03

19 – Mesut Ozil (2015-16)

Mchezaji mwingine wa Arsenal, Mesut Ozil, aliongoza kwa asisti katika msimu wa 2015-16, akiwa na 19 katika mechi 35 za ligi.

Asisti 16 kati ya hizo zilikuja katika michezo yake 18 ya kwanza ya msimu huo, huku kiungo huyo wa Ujerumani akionekana kuwa karibu kuvunja rekodi ya Henry ya asisti 20.

Lakini michezo 17 ya mwisho ya msimu huo ilizaa asisti tatu tu zaidi, ikiwemo moja katika siku ya mwisho ya msimu katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Aston Villa.

Idadi ya Ozil ya msimu wa 2015-16 ilikuwa mbili zaidi kuliko aliyowahi kufikia katika msimu mmoja akiwa Real Madrid kwenye La Liga, ambapo asisti zake 17 katika misimu ya 2010-11 na 2011-12 zilikuwa kiwango chake cha juu nchini Hispania.

ASIS 04

18 – Mohamed Salah (2024-25)

Mohamed Salah alifikisha asisti 18 kwa Liverpool msimu wa 2024-25 wa Ligi Kuu England kupitia krosi yake ya chini iliyomsaidia Luis Díaz kufunga bao la kwanza dhidi ya West Ham United, Aprili 13, 2025.

Hata hivyo, alishindwa kuongeza nyingine katika michezo sita ya mwisho ya msimu na kumaliza akiwa pungufu ya mbili kufikia rekodi ya msimu huo katika mashindano hayo.

Mmisri huyo ambaye alisaini mkataba mpya na klabu hiyo ili kuendeleza maisha yake Ligi Kuu England zaidi ya 2024-25 kabla ya huu kutangaza kwamba anaondoka, alifurahia msimu wake bora zaidi wa asisti katika mashindano hayo. Idadi yake ya juu kabla ya hapo ilikuwa katika msimu wa 2021-22 alipotoa asisti 13.

ASIS 05

18 – Cesc Fàbregas (2014-15)

Akiwa Arsenal katika msimu wa 2007-08, Cesc Fabregas alitoa asisti 17 za kuvutia. Ilikuwa vigumu kwa mashabiki wa Arsenal kumuona kiungo wao wa zamani akiishia Chelsea kupitia Barcelona baada ya hapo, lakini ilikuwa ngumu zaidi walipomuona akifanya vizuri Stamford Bridge.

Katika msimu wa 2014-15, Fabregas ambaye anashika nafasi ya tatu kwa asisti nyingi zaidi za muda wote katika Ligi Kuu akiwa na 111 alizidi kiwango chake hicho cha awali na kufikisha asisti 18 kwa Chelsea, tena katika michezo 34 tu ya ligi. Chelsea walitwaa ubingwa kwa urahisi msimu huo, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania aliongoza kwa mbali orodha ya asisti nyingi zaidi, akimaliza akiwa na tofauti ya saba mbele ya aliyemfuata kiungo mwingine Mhispania wa Arsenal, Santi Cazorla (11).

ASIS 06

18 – Kevin De Bruyne (2016-17)

Kama ilivyokuwa msimu wa 2019-20, De Bruyne alifanya vizuri licha ya timu yake kutofanya vizuri sana. Katika msimu wa kwanza wa kocha Pep Guardiola nchini England, Manchester City hawakuwa karibu kushindania ubingwa, ambao ulichukuliwa na Chelsea ya zamani ya De Bruyne kwa tofauti kubwa, lakini mchezaji huyo bado aliweza kufikisha asisti 18 kwa wenzake katika michezo 36.

Hiyo ilikuwa tatu zaidi ya Christian Eriksen wa Tottenham Hotspur, lakini kama tulivyoona tayari, De Bruyne alikuja kufanya vizuri zaidi miaka mitatu baadaye.

ASIS 07

18 – Frank Lampard (2004-05)

Pale ambapo kuna rekodi za Ligi Kuu England, jina la Frank Lampard haliko mbali. Kiungo huyo wa zamani wa West Ham, Chelsea na Manchester City anashika nafasi ya tano katika orodha ya muda wote ya asisti za Ligi Kuu England, na msimu wa 2004-05 ulikuwa bora zaidi kwake.

Chelsea walitwaa ubingwa kwa urahisi chini ya Jose Mourinho katika msimu wake wa kwanza Stamford Bridge, na Lampard alikuwa sehemu kubwa ya mafanikio hayo, akifunga mabao 13 pamoja na kutoa asisti 18.