EPL na hesabu za vidole Ligi ya Mabingwa Ulaya
Muktasari:
- Kadri mwisho wa msimu unavyokaribia, ni wakati wa kuelewa kanuni zinazozidi kuwa tata zinazoamua kama klabu yako itafuzu kucheza Ulaya.
LONDON, ENGLAND: NAFASI za kushiriki mashindano ya Ulaya kutoka Ligi Kuu England msimu ujao bado zinabadilika-badilika, jambo linaloacha msisimko mkubwa hadi siku ya mwisho ya kipute cha ligi hiyo bora zaidi Ulaya kwa sasa.
Kadri mwisho wa msimu unavyokaribia, ni wakati wa kuelewa kanuni zinazozidi kuwa tata zinazoamua kama klabu yako itafuzu kucheza Ulaya.
Lakini, jambo moja la hakika; kutakuwa na angalau timu nane za England zitakazocheza mashindano ya bara hilo msimu ujao, na huenda zikawa zaidi. Habari mbaya ni kwamba kama unamiliki mtandao wa klabu nyingi, umechelewa kuweka hisia zako kwenye moja.
NAFASI NGAPI KLABU ZA ENGLAND?
Kwa sasa ni nane. Zinagawanyika kama ifuatavyo: Kuna nafasi nne za Ligi ya Mabingwa Ulaya zinazotolewa kulingana na nafasi ya ligi pamoja na nafasi ya tano iliyohakikishiwa kutokana na mafanikio ya ligi hiyo Ulaya msimu huu; nafasi mbili za Europa League, moja kupitia ligi na nyingine kwa mshindi wa FA ilhali kuna nafasi ya mwisho ya kufuzu Conference League inayotolewa kwa timu mojawapo ya ligi na kwa mshindi wa Carabao.
Lakini, kama Ligi Kuu England ingeisha leo, nani angefuzu na kwenda wapi? Manchester City, Arsenal, Manchester United, Aston Villa na Liverpool wangeshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mujibu wa nafasi zao, huku nafasii ya sita kwa sasa Brighton ingeenda Europa League na nafasi ya saba Bournemouth ingeenda Conference League.
Nafasi ya mwisho; ile ya pili ya Europa League inayohusiana na FA itaamuliwa baadaye. Lakini kama Manchester City watashinda kombe hilo nafasi hiyo itashuka kwenye ligi, kumaanisha kuwa nafasi ya sita na ya saba zitakwenda Europa League na nafasi ya nane itaenda Conference League.
Hii kwa sasa ingemaanisha Chelsea, ambao bila shaka wangefurahia nafasi ya kurejesha taji waliloshinda msimu uliopita.
Je kunaweza kuwapi zaidi ya hapo? Ndiyo, lakini inategemea sana Aston Villa. Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) huwapa washindi wa Europa League nafasi ya moja kwa moja kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya - nafasi ambayo inaweza kwenda kwa Aston Villa au Nottingham Forest.
Vivyo hivyo, ikiwa Crystal Palace watashinda Conference League watapata nafasi ya Europa League. Hivyo jumla inaweza kufika timu 10 kati ya 20 za Ligi Kuu England zikacheza mashindano ya Ulaya msimu ujao.
Lakini, kuna mambo ya ziada; ikiwa Villa watashinda Europa League, lakini wakamaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye ligi, hakuna nafasi ya ziada ya Ligi ya Mabingwa kulingana na sheria za UEFA.
Hata hivyo, kutokana na namna UEFA inavyotoa nafasi ikiwa Villa watashinda na kumaliza nafasi ya tano au chini, basi nafasi ya sita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itapatikana na kushuka hadi kwenye jedwali la ligi.
Wakati huohuo, nafasi hiyo ya sita ya Ligi ya Mabingwa inaondoa nafasi ya Europa League ambayo ingepewa kupitia ligi.
Hakuna matatizo kama hayo ikiwa Nottingham Forest watashinda; kutokana na nafasi yao ya sasa, hiyo itakuwa ongezeko la moja kwa moja (+1).
AJABU ZAIDI INAWEZA KUWA IPI?
Kati ya nafasi ya sita na ya 12 kwenye Ligi Kuu England kuna tofauti ya pointi tano tu, hivyo kuna uwezekano mwingi ambapo timu isiyotarajiwa sana kama Fulham au Sunderland inaweza kupata nafasi ya Ulaya dhidi ya timu kubwa zaidi kama Chelsea.
Kuna pia uwezekano wa ajabu na Brentford wanaweza kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kwa kupoteza mechi yao ya mwisho!
Hebu chukulia hivi, Aston Villa washinde Europa League katikati ya wiki kabla ya raundi ya mwisho ya mashindano hayo.
Na Brentford wawe wameshinda mechi dhidi ya Brighton na Bournemouth, na hawawezi kushuka chini ya nafasi ya sita. Kisha watalazimika kutumaini kuwa Villa wanamaliza nafasi ya tano ili nafasi ya ziada ya Ligi ya Mabingwa ishuke hadi kwao.
Habari njema kwa Brentford ni kwamba Aston Villa wanacheza na Manchester City siku ya mwisho, huku wao wakisafiri kucheza na Liverpool, timu iliyo nafasi ya tano kwa sasa.
Pointi tatu kwa Liverpool zinaweza kuwapa Brentford nafasi ya ndoto zao ya kucheza mashindano ya Ulaya, wakati ushindi wao wenyewe unaweza kuimaliza ndoto hiyo. Hali hiyo inaleta taswira isiyo ya kawaida, lakini huenda mambo yasifikie hatua hiyo.