Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BADO KIDOGO…! Man United yasikilizia mbili tu kufuzu Uefa

MAN Utd Pict

Muktasari:

  • United inaweza kuthibitisha kufuzu endapo itashinda mechi zake mbili zijazo dhidi ya Brentford na Liverpool. Ushindi huo utaifanya isiweze kufikiwa na wapinzani wake, bila kujali matokeo mengine.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United iko katika nafasi nzuri ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Chelsea. Timu hiyo ya Michael Carrick sasa inaongoza kwa pointi 10 dhidi ya Chelsea, huku zikiwa zimesalia mechi tano.

United inaweza kuthibitisha kufuzu endapo itashinda mechi zake mbili zijazo dhidi ya Brentford na Liverpool. Ushindi huo utaifanya isiweze kufikiwa na wapinzani wake, bila kujali matokeo mengine.

Hata hivyo, kama haitafanikisha hilo mapema, bado itahitaji kushinda mechi dhidi ya Nottingham Forest, Sunderland na Brighton ili kujihakikishia nafasi hiyo muhimu ya Ulaya.

Baada ya mchezo huo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Carrick alikisifu kikosi chake kwa kuwa imara kiakili na kusisitiza walistahili kushinda kwa namna yoyote.

Bao la Matheus Cunha, lililotokana na pasi ya kapteni Bruno Fernandes aliyekuwa kwenye kiwango bora, ndilo lililoamua mchezo huo na kuifanya Man United kuimarisha nafasi yao katika mbio za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Baada ya kupoteza mechi hiyo, Chelsea rasmi inakuwa imepokea kichapo cha nne mfululizo katika Ligi Kuu England jambo ambalo halijawahi kutokea tangu mwaka 1927.

Akizungumza katika kipindi cha Match of the Day baada ya mechi hiyo, Carrick amesema: “Naamini tulistahili ushindi huu. Changamoto tulizokutana nazo siku chache zilizopita, hasa kwenye safu ya mabeki wa kati, zilifanya hali iwe ngumu, lakini ulinzi katika hali isiyo ya kawaida, tulionyesha uimara sana katika eneo hilo."

"Tulikuwa hatari kwenye mashambulizi ya kushtukiza. Ili kuja hapa na kushinda, tulihitaji nidhamu na namna wachezaji walivyopambana ilikuwa ni kwa asilimia kubwa sana leo. Tumepata ushindi na tunafurahi sana."

Ingawa Cunha ndiye aliyefunga bao la ushindi, Fernandes alipata sifa nyingi kwa kiwango chake cha juu  akionekana kuchezesha timu na kusaidia katika kujilinda.

Nyota huyo wa Ureno alitoa pasi ya bao na kuwa tishio muda wote kwa Chelsea, hali iliyomfanya atangazwe mchezaji bora wa mechi.

Baada ya mechi Fernandes amesema: “Ni jambo  zuri sana kwetu, tulihitaji kurejea kwenye hali ya kushinda. Sio tu kutokaa na kile kilichotokea mechi dhidi ya Leeds, tulikuwa na michezo miwili hatukushinda. Tulijua tunahitaji kucheza vizuri kwa sababu Chelsea ni timu nzuri. Lengo letu ni kumaliza nafasi nne za juu."

Kwa upande wa kocha wa Chelsea, Liam Rosenior, kipigo hicho kinaongeza presha baada ya timu yake kupoteza mechi nne mfululizo za ligi bila kufunga bao

Licha ya kutengeneza nafasi nyingi, walishindwa kupenyeza mpira wavuni, jambo lililowaacha mashabiki wao wakiondoka uwanjani wakiwa na hasira.

Rosenior amesema: “Ni hali ngumu sana. Leo walipiga shuti moja tu lililolenga lango, wakati sisi tulishambulia mara kwa mara na hata kugonga mwamba wa goli mara kadhaa. Hatupaswi kuhisi kama mambo yako vibaya sana, tunapaswa kuendelea kupambana. Kwa sasa, makosa madogo yanatuadhibu na hilo linapaswa kubadilika.”