Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United kuuza mastaa watano

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa takribani wachezaji wanne wa Man United wanatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu kwa kuuzwa mbali ya wale ambao mikataba yao itamalizika.

MANCNESTER, ENGLAND: TAJIRI wa Manchester United,  Jim Ratcliffe anataka kiasi cha Pauni 100 milioni  kutokana na mauzo ya wachezaji dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hadi sasa takribani wachezaji wanne wa Man United wanatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu kwa kuuzwa mbali ya wale ambao mikataba yao itamalizika.

Manuel Ugarte, Joshua Zirkzee, Andre Onana, Rasmus Hojlund na Marcus Rashford ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuuzwa, huku Casemiro, Jadon Sancho na Tyrell Malacia wataondoka kama wachezaji huru, jambo litakalosaidia kupunguza mzigo wa mishahara.

Man United wanatarajia kupata hadi Pauni 64 milioni kutokana mauzo ya  Marcus Rashford na Rasmus Hojlund iwapo Barcelona na Napoli zitaamua kuwasajili mazima.

Vilevile wanaweza wakapata Pauni 19 milioni kwa ajili ya kipa Andre Onana ambaye anacheza kwa mkopo Trabzanspor ya Uturuki.

Mashetani Wekundu wanaweza kupata hasara kwa Manuel Ugarte aliyenunuliwa kwa Pauni 50.8 milioni na Joshua Zirkzee aliyenunuliwa kwa Pauni 36.5 milioni  kwani wanaweza kuuzwa kwa bei za chini zaidi.

Hata hivyo, kuondoka kwa Casemiro anayelipwa Pauni 350,000 kwa wiki kutasaidia sana kupunguza matumizi ya kikosi na kuongeza uwezekano wa kusajili mastaa kwa bei kubwa kidogo.

Hatua hii ya kusafisha kikosi inakuja wakati Man United ikionyesha nia kubwa ya kumsajili nyota wa kimataifa wa England, Elliot Anderson.

Kiungo huyo wa Nottingham Forest anadaiwa kuwa anauzwa kwa takribani Pauni 100 milioni na timu yake na ikiwa ataenda kuonyesha kiwango bora katika michuano ya Kombe la Dunia akiwa na England mwaka huu bei inaweza kupanda zaidi.

Hata hivyo, mabosi wa Man United wanaamini bei ya Pauni 100 milioni inaweza kushuka na wanapambana kufanya makubaliano ya kumsajili kabla hajaenda kucheza Kombe la Dunia.

Wapinzani wao Manchester City pia wanapanga kumsajili Elliot ili akawe mbadala wa Bernardo Silva, anayetarajiwa kuondoka mwisho na wanaonekana kuwa mstari wa mbele katika dili hilo.