Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kuwa ya nne Afrika ni udhaifu CAF, kama ilivyokuwa FIFA, Jamhuri Ya Czech 2006

PUMZI Pict

Muktasari:

  • Orodha hii ilisababisha ukosoaji mkubwa sana kutoka kwa walumbi. Watu walihoji inawezekanaje Jamhuri ya Czech kupanda hadi nafasi ya pili ilhali haikuwa na maajabu yoyote.

KUELEKEA Kombe la Dunia 2006, Shirikisho la soka la Kimataifa, FIFA, lilitoa orodha ya viwango vya ubora wa kila nchi duniani.

Katika orodha hiyo iliyoongozwa na Brazil, Jamhuri ya Czech, nchi ambayo haikuwa na mafanikio yoyote, ikashika nafasi ya pili.


Hii ni orodha ya 10 bora ilikuwa kama ilivyotolewa na FIFA, Mei 2006:

1. Brazil (alama 827, bara Amerika Kusini/CONMEBOL)

2. Jamhuri ya Czech (alama 772, bara Ulaya/UEFA)

3. Uholanzi (alama 768, bara Ulaya/UEFA)

4. Mexico (alama 758, bara Amerika Kaskazini/CONCACAF)

5. Marekani (alama 756, bara Amerika Kaskazini/CONCACAF)

5. Hispania (alama 756, bara Ulaya/UEFA)

7. Ureno (alama 750, bara Ulaya/UEFA)

8. Ufaransa (alama 749, bara Ulaya/UEFA)

9. Argentina (alama 746, bara Amerika Kusini/CONMEBOL)

10. England (alama 741, bara Ulaya/UEFA)


PUMZ 01
PUMZ 01

Orodha hii ilisababisha ukosoaji mkubwa sana kutoka kwa walumbi. Watu walihoji inawezekanaje Jamhuri ya Czech kupanda hadi nafasi ya pili ilhali haikuwa na maajabu yoyote.

Na hata yalipoanza mashindano, nchi hiyo ilitolewa hatua ya makundi, tena kwa fedheha sana.

Mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi walifungwa 2-0 na Italia ambayo ilikuwa katika nafasi ya 13.

Miongoni mwa wakosoaji wakubwa walikuwa watu wawili wataalamu wa mahesabu, takwimu na ukokotoaji, bwana Bylan McHale na bwana Stephen Davies.

Mabwana hawa wakauchambua mchakato wa FIFA wa kupanga viwango na kuja na hitimisho kwamba njia ambazo FIFA ilikuwa ikizitumia hadi mwaka 2006 zilikuwa na chembechembe nyingi za kukosa uhalisia.

SIMBA 01

Mfumo wa kawaida wa utoaji alama kwa timu hutegemea matokeo ya uwanjani, yaani ushindi, sare au kupoteza.

Lakini hadi wakati huo, FIFA walikuwa hawaamini kama matokeo ya uwanjani pekee, yaani ushindi, sare au kupoteza, yangetosha kutoa viwango sahihi na vya kuaminika.

Hivyo kwenye ukokotoaji wao wakaongeza vigezo vingine vilivyozingatia uimara au ubora wa mpinzani.

Yaani timu ndogo ikiifunga timu kubwa ambayo ni imara na ina ubora mkubwa, basi inapata alama nyingi zaidi…kuliko zile za kawaida yaani tatu kwa kushinda, moja kwa sare au sifuri kwa kufungwa

Hii ikasababisha alama nyingi zaidi kuvunwa na timu ndogo kwa kushinda dhidi ya timu kubwa na bora kuliko kushinda dhidi ya timu dhaifu.

Yaani ingekuwa ndiyo kwenye ligi yetu, basi KenGold ambayo ni ya mwisho kwenye msimamo inapata alama nyingi zaidi kwa kuifunga Yanga inayoongoza ligi, kuliko  wakiifunga Kagera Sugar.

SIMBA 02

Pia kanuni za ukokoatji za FIFA ziliziwezesha timu dhaifu kupata alama mbele ya timu bora hata kama zimepoteza mchezo, eti kwa kigezo cha kucheza vizuri (endapo zitapata angalau goli moja au zikifungwa kwa idadi ndogo ya mabao).


Na endapo mechi iliamuliwa kwa mikwaju ya penalti, basi timu iliyoshinda itapata alama za ushindi na iliyopoteza itapata alama za sare kwa sababu walilazimisha sare hadi kufikia hatua ya mikwaju ya penalti.

FIFA walianza kutoa orodha ya viwango kwa timu za taifa za wanaume kuanzia mwaka 1993 wakitumia njia hizi ambazo kidogo zilifanyiwa marekebisho 1999.

Lakini balaa la Jamhuri ya Czech la 2006 likaifanya FIFA ibadili tena njia zake mwaka huo…na ikabadili tena 2018.

Mkasa wa FIFA na Jamhuri ya Czech 2006 unaotaka kufanana na huu wa Simba kuwa klabu ya nne kwa ubora barani Afrika. 

SIMBA 03

Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya mtandao wa kijamii wa africasoccerzone ambao ulinukuu taarifa mpya za CAF baada ya Simba kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Hata hivyo, kwenye mitandao yote ya CAF taarifa hizo hazikuwepo.


Ifuatayo ni orodha ya 10 bora:

1. Al Ahly (alama 78, nchi Misri)

2. Mamelodi Sundown (alama 57, nchi Afrika Kusini)

3. Esperance (alama 57, nchi Tunisia)

4. Simba (alama 43, nchi Tanzania)

5. RS Berkane (alama 42, nchi Morocco)

6. Zamalek (alama 42, nchi Misri)

7. Wydad (alama 39, nchi Morocco)

8. Pyramids (alama 37, nchi Misri)

9. USM Alger (alama 37, nchi Algeria)

10. CR Belouizdad (alama 36, nchi Algeria)

Hili ni jambo la kustaajabisha sana ukizingatia Simba hawana chochote walichoshinda barani Afrika, na hata ndani ya nchi.

Mafanikio ya Simba barani Afrika ni robo fainali, ukiacha nusu fainali ya mwaka huu. Timu ambazo ziko chini ya Simba zina mafanikio makubwa kuliko Simba…ajabu!

Nitatumia mafanikio ya miaka mitano iliyopita, kama ya msimu huu wa mashindano ambao unaendelea, kuanzia 2020.

SIMBA 04

Nafasi  Klabu  Ligi ya mabingwa, Kombe la shirikisho, CAF Super Cup, AFL

4. Simba 2020 – Raundi ya Awali

2021 – Robo fainali 2022 – Raundi ya pili

2023 – Robo fainali 2024 – Robo fainali 2022- Robo fainali

2025 – nusu fainali - Nusu fainali


5. Berkane 2020 – Mabingwa

2021 – Makundi

2022 – Mabingwa

2023 – Mtoano

2024 – Fainali

2025 – Nusu fainali

2021 – Fainali

2022 – Mabingwa

           

6. Zamalek 2021 – Makundi

2022 - Makundi

2023 – Makundi

2024 - Mabingwa

2025 – Robo fainali     2020 – Mabingwa

2024 – Mabingwa

           

7.  Wydad 2021 – Nusu fainali

2022 – Mabingwa 2023 – Fainali

 2024 - Makundi          -           2022 - fainali   2023 - Fainali


Katika kanuni zote za kupima viwango vya timu, matokeo ambayo hutumika ni ya kipindi cha miaka mitano, yanaitwa 5 year ranking.

Sasa ukiangalia matokeo ya miaka mitano ya timu hizi ambazo ziko chini ya Simba, unaona zina mafaniko makubwa zaidi ya Simba.

SIMBA 05

Hakuna namna yoyote ya kawaida ambayo itaifanya Simba iwe juu ya hawa…lakini mtandao wa africasoccerzone unasema Simba yuko juu yao.

Hapo ndipo tunapotilia shaka taratibu za michakato yao, kama ilivyokuwa kwa FIFA na Jamhuri ya Czech mwaka 2006.