‘Bahati yao hao tungewafunga’

Kiungo wa Chelsea, Ramires (kulia) akidhibitiwa na straika wa Manchester United, Wayne Rooney, Old Trafford jana Jumatatu usiku.
Muktasari:
Moyes alimwanzisha Wayne Rooney kwenye mechi hiyo katika kikosi chake cha kwanza huku akijua kuwa kocha Mourinho anamtaka lakini alimwingiza uwanjani na kumwambia: “Cheza mpira.”
Bahati yao ndiyo maneno waliyokuwa wakitambiana makocha, David Moyes wa Manchester United na Jose Mourinho wa Chealsea baada ya suluhu ya timu hizo jana jumatatu usiku kwenye ligi kuu ya England, Tambo na mbwembwe nyingi za makocha hao zilikoma.
Moyes alimwanzisha Wayne Rooney kwenye mechi hiyo katika kikosi chake cha kwanza huku akijua kuwa kocha Mourinho anamtaka lakini alimwingiza uwanjani na kumwambia: “Cheza mpira.”
Akafanya hivyo, licha mashabiki waliojazana Old Trafford walimchanganya kidogo kutokana na pande zote mbili kumshangilia kila alipogusa mpira. Waliita ‘’Rooney, Rooney!’
Swali la nani zaidi Mourinho na Moyes kwenye mechi hiyo lilikosa jibu na baada ya mechi kila mmoja alitoa sababu za kumkosakosa mwenzake.
Kwenye dakika hizo 45 za kipindi cha kwanza, Manchester United walimiliki, huku wenzao wa Chelsea wakicheza kwa kimbinu zaidi. Mbrazili, Oscar alimkosa mara kadha kipa David De Gea kwa mashuti makali.
Kwa matokeo hayo Manchester United imeshindwa kufuta uteja kwani katika mechi tano kabla ya mchezo huo wa jana Jumatatu, ilishinda mara moja tu, wakati ilipoinyuka Chelsea kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge mabao 3-2, Oktoba 28, mwaka jana huku The Blues wakishinda mara tatu na kutoka sare moja.
Baada ya kumaliza kibarua hicho, Manchester United Jumapili ijayo itakuwa na shughuli pevu Anfield wakati itakapokwenda kuifuata Liverpool, wakati Chelsea wao watakipiga na Bayern Munich katika mechi ya European Super Cup, Jumamosi ijayo.
Manchester United: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Cleverley, Valencia/Young, Rooney, Welbeck/Giggs, Van Persie.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard; De Bruyne/Torres, Oscar, Hazard/Azpilicueta, Schurrle/Mikel.