Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yapeleka ubabe Kanda ya Ziwa

VINARA wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), Yanga Princess imetamba inataka kumaliza duru la kwanza ikiwa kileleni tena bila kupoteza mchezo na kusisitiza inaenda kuvuna pointi zote sita katika michezo miwili watakayocheza Kanda ya Ziwa wiki hii.

Timu hiyo itaanza harakati zake za kupata pointi hizo sita kwa kucheza na TSC Queens kesho Jumanne kwenye uwanja wa CCM kirumba Mwanza na Ijumaa itaikabili Alliance Girls kwenye uwanja wa Nyamgana Mwanza.

Baada ya michezo hiyo, ligi ya wanawake itakuwa mapumziko hadi Februari 15 itakaporejea tena kwa Yanga Princess kuwa ugenini kuivaa Tanzanite mkoani Dodoma.

Kocha msaidizi wa Yanga Princess, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ alisema wamepania kumaliza mzunguko wa kwanza bila kupoteza na anaamini jambo hilo watalitimiza.

“Tumepania msimu huu na ndio maana kila mechi kwetu tunaichukulia kama fainali na nawashukuru wachezaji wanapambana na kupata ushindi.

“Tunataka tumalize mzunguko wa kwanza tukiwa kileleni tena tukiwa timu ambayo haijapoteza mchezo na namaini hilo litafanikiwa.

“Tunajua mechi hizo mbili za Kanda ya ziwa zitakuwa ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi na kutimiza lengo letu la kumaliza mzunguko wa kwanz atulkiwa bado tunaongoza ligi,” alisema Mmachinga.

Yanga Princess inaongoza ligi ya wanawake ikia na pointi 25 baada ya kucheza michezo tisa, imeshinda nane na kutoka sare mchezo mmoja.

Timu hiyo imeonekana iko vizuri zaidi hasa eneo lake la ulinzi kwani imeruhusu bao moja tu mpaka sasa huku ikibebwa zaidi eneo la ushambuliaji na starika ao matata, Aisha Massaka mwenye mabao tisa.