Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BDL ni mwendo wa maokoto, ubora

BDL Pict

Muktasari:

  • Timu ya Dar City inamilikiwa na  Mussa Mzenji, huku Stein Warriors ikiwa mikononi mwa Karabani Karabani na mbali ya kumiliki timu hizo kila moja ina benchi la ufundi lenye uwezo mkubwa wa kuisimamia.

WAKATI timu zikitafuta wawekezaji wa kuzisapoti katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), imeonyesha kuwa Dar City na Stein Warriors ndizo pekee zilizopata wawekezaji. 

Timu ya Dar City inamilikiwa na  Mussa Mzenji, huku Stein Warriors ikiwa mikononi mwa Karabani Karabani na mbali ya kumiliki timu hizo kila moja ina benchi la ufundi lenye uwezo mkubwa wa kuisimamia.

Timu hizo pia zimesajili wachezaji wenye uwezo mkubwa pamoja na kuwasainisha mikataba inayofanya walipwe mishahara  tofauti na timu zingine.

Kwa upande wa Dar City, baadhi ya wachezaji iliowaongezea mikataba ni Erick John, Ally Abdallah na Stanley Mtunguja iliyemsajili kutoka Ukonga Kings. Wachezaji hao pia waliambatana na timu hiyo kwenda nchini Rwanda kushiriki mashindano ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari.

Upande wa Stein Warriors imemsajili Jonas Mushi na Felix Luhamba kutoka JKT, Evance Davies, Tyrone Edward na Mwalimu Heri waliokuwa wakikipiga UDSM Outsiders. Mbali na timu hizo kupata wawekezaji,  timu zinazotoka katika taasis kama JKT, ABC, Polisi, Chui na Mgulani JKT zinapata sapoti kutoka  maeneo yao ya kazi, hivyo kuzirahisishia katika suala la maokoto.

BD 01

DAR CITY HAITAKI UTANI

Kama hujui ni kwamba Dar City imemchukua nyota wa timu ya APR ya Rwanda, Obadiah Noel kwa ajili ya kuichezea katika BDL.

Noel anayecheza namba 1 maarufu kama point guard ambapo katika mashindano ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari, Rwanda alichezea Dar City.

Raia huyo wa Marekani alishirikiana na wachezaji wengine wa kimataifa kina Deng Dheu, raia wa Sudan anayeishi Marekani pamoja na Mtanzania Hasheem Thabeet.

Nyota huyo aliiwezesha Dar City kucheza nusu fainali baada ya kuongoza kwa kufunga pointi 22 katika mchezo wao na timu ya Patriots kwa pointi 22.

BD 02

WAKONGWE WA HIZI KAZI

Licha ya timu kongwe za Vijana, Kurasini, Pazi na Savio kutokuwa na wawekezaji, zina uzoefu wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) na huenda ukazibeba.

Vijana maarufu kama City Bulls katika Ligi hiyo imejiwekea utaratibu wa kusajili wachezaji wanaotoka kikosi chake cha pili kiitwacho Jogoo.

Kwa upande wa Kurasini Heat iliyopanda daraja mwaka huu inaonekana kujipanga vizuri kurudisha heshima iliyopotea miaka mitano iliyopita, baada ya kushuka daraja 2020. 

Nayo Pazi ambayo katika ligi ya mwaka jana haikufanya vizuri, lakini katika ligi ya mwaka huu inaonyesha kuanza kujipanga baada ya kuanza usajili kwa kumsajili Sam Agutu na Jovin Ngowi walitokea Mchenga Star na Srelio mtawalia.

Upande wa timu ya Savio, wachezaji wazawa ndiyo wanaoonekana kuwa huenda wakaibeba ambao ni pamoja na Oscar Mwituka, Corelius Mgaza Jamal Salumu na Yunzu Maige waliowahi kukiwasha na kung'ara katika misimu iliyopita.

BD 03

UDSM OUTSIDERS

Timu ya UDSM iliyotolewa na JKT katika fainali ya BDL msimu uliopita kwa michezo 3-1 ipo kimyakimya, lakini ikionyesha kwamba  makali ni kama yamepungua kutokana na wachezaji wake nyota Tryone Edward, Evance Davies na Mwalimu Heri kutimkia Stein Warriors.

Hata hivyo, katika BDL imejipanga kuziba nafasi za wachezaji hao kwa kusajili nyota  kutoka kikosi chake cha pili  maarufu kama Crowns.

BD 04

MCHENGA STAR

Baada ya Mchenga Star kufanya vizuri katika ligi hiyo mwaka jana, imetikisika ni baada ya baadhi ya wachezaji wake kutimkia JKT, ABC na Pazi.

Wachezaji hao ni Sam Agutu aliyetimkia Pazi, Meshack Edward (ABC) na Jordan Manag (JKT).

BD 05

KIUT, DB ORATORY

Timu hizo zinatakiwa zijipange vizuri kuhimili mikikimikiki BDL mwaka huu, huku KIUT iliyonusurika kushuka daraja mwaka jana, huenda isifanye usajili wa wachezaji kutoka nje ya chuo hicho (Kampala International University).

KIUT licha ya kuonyesha kiwango bora katika mashindano ya vyuo huenda ikwa na wakati mgumu katika kutoa ushindani BDL mwaka huu endapo haitaongeza wachezaji.


BD 06

DB ORATORY

Licha ya timu hiyo kushika nafasi ya tisa katika BDL kwa pointi 39, inatakiwa ifanye kazi kubwa kumili mikikimikiki ya ligi hiyo. Timu hiyo inayosimamiwa na Kituo cha Donbosco - Oysterbay, inapaswa iongoze wachezaji katika ligi hiyo.