Dar City si haba Rwanda

Muktasari:
- Katika mchezo huo Aliou Diarra alifunga pointi 18 akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Axel Mpayo aliyefunga 12.
TIMU ya APR ya Rwanda imeifunga Dar City kwa pointi 81-68 katika nusu fainali ya mashindano ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Petit Gymnasium nchini Rwanda.
Katika mchezo huo Aliou Diarra alifunga pointi 18 akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Axel Mpayo aliyefunga 12.
Kwa upande wa Dar City alikuwa ni Deng Dheu aliyefunga pointi 28 akifuatiwa na Kylian Rotardier aliyefunga 14.
Kuingia nusu fainali kwa Dar City kulikuja baada ya timu hiyo kuifunga timu ngumu ya Patriots ya Rwanda kwa pointi 76-64.
Katika mchezo huo Obadiah Noel alifunga pointi 22 akifuatiwa na Deng Dhieu aliyefunga 21, huku Cle Elliot wa Patriots akifunga pointi 14. Katika fainali APR iliifunga United Generatin (UGB) kwa pointi 94-92.