Adebayor kuanza na Tanzania Prisons

Muktasari:
- Timu hiyo ilimsajili Adebayor kutoka Niger, kutokana na CV ya jina lake wengi walitarajia angekuwa miongoni mwa nyota ambao wangefanya vizuri ila haikuwa hivyo.
MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars, Victorien Adebayor ambaye tangu asajliwe dirisha kubwa la msimu huu hajaonekana uwanjani, inaelezwa huenda akaanza kuitumimi imu hiyo jkatika mechi ya Luigi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kufanya mazoezi na kuingia katika mfumo wa kocha.
Timu hiyo ilimsajili Adebayor kutoka Niger, kutokana na CV ya jina lake wengi walitarajia angekuwa miongoni mwa nyota ambao wangefanya vizuri ila haikuwa hivyo.
Mkurugenzi Idara ya Utawala wa Singida, Mhibu Kanu alithibitisha Adebayor kuwepo katika programu ya kucheza mechi ya mwisho ya kufunga duru la kwanza dhidi ya Prisons, kutokana na kocha kuona utayari wa kuisaidia timu.
“Kafanya mazoezi takribani wiki tatu, ikumbukwe alikotoka alikuwa hachezi, ndio maana kulikuwa na ukimya kumhusu, ila kwa sasa mtamuona sana, “ alisema Kanu na kuongeza;
“Natarajia atafanya makubwa, kwani ni mchezaji mzuri na ana CV kubwa, ingawa mzunguko wa pili ndio atakuwa na nafasi ya kucheza mechi nyingi.”
Jina la Adebayor, lilianza kugonga vichwa vya habari nchini mwaka 2022 baaada ya kuonekana akiwa na kikosi cha Union Sportive de la Gendarmerie N ationale maarufu kama USGN ya Niger katika Kombe la Shirikisho, huku akihusishwa kutakiwa na Simba, ila dili lilikufa baada ya kuibukia RS Berkane ya Morocco.