Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: Mzee Mangungu anastahili pongezi Simba

MANGUNGU Pict

Muktasari:

  • Huyu ni Murtaza Mangungu mwenyekiti wa klabu hiyo. Mkiona nimemuita Mwinyi msiniige maana yule ni mtani wangu. Wangindo na Wamwera ni watani sasa kama humtanii muite tu Mangungu.

MWINYI mmoja kutoka Kilwa sasa hivi anaweza kuwa miongoni mwa wanadamu wenye furaha sana pale ndani ya Simba kutokana na mwenendo mzuri wa timu hiyo.

Huyu ni Murtaza Mangungu mwenyekiti wa klabu hiyo. Mkiona nimemuita Mwinyi msiniige maana yule ni mtani wangu. Wangindo na Wamwera ni watani sasa kama humtanii muite tu Mangungu.

Mtani wangu ni lazima awe na furaha maana kipindi fulani alishambuliwa sana na baadhi ya wanachama na mashabiki wake wengine wakisema ni Yanga, huku kukiwa na waliosema hatoshi kuiongoza Simba.

Kwa sisi hapa mtaani tulifahamu zile zilikuwa hasira za Simba kutofanya vizuri kwenye mashindano ambayo inashiriki. Mashabiki wa soka la bongo tunajuana buana kila timu inapofanya vibaya lazima atafutwe mtu wa kuangushiwa lawama hata kama hausiki.

Lakini chuma Mangungu kilisimama imara na hakikuyumbishwa na kelele ambazo zilikuwa zinapigwa juu yake maana alitambua wanaomlaumu wanashindwa kulinyooshea kidole tatizo halisi ambalo lilikuwa ni ubora mdogo wa kikosi chao.

Dirisha la usajili yeye na viongozi wenzake kwa kushirikiana na benchi la ufundi wakafanya usajili wa wachezaji wazuri na washindani huku wakiimarisha benchi lao la ufundi kwa kumchukua kocha Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini.

Wakaipeleka timu Misri ambako ilipata maandalizi bora ya kabla ya msimu (pre season) na kisha wakacheza mechi za ushindani za kirafiki ambazo zililipa fursa benchi la ufundi kung’amua mapungufu na kuyafanyia kazi mapema.

Matunda yake yanaonekana katika ligi ambapo ipo nafasi ya pili na katika mashindano ya kimataifa imeingia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na ina uwezekano mkubwa wa kuingia fainali kama mambo yakiwaendea vizuri kule Afrika Kusini.

Kumbe kipindi kile walikuwa wanamuonea bure mtani wangu kumlaumu kuwa yeye ni Yanga ila uhalisia ni hawakuwa na wachezaji wengi wenye ubora. Si unaona sasa wanatamba tu wamesahau hata kumuomba msamaha.