Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Azam yawazidi nguvu Cannavaro, Twite

Azam FC ya jijini Dar es Salaam, timu inayoonyesha muelekeo mzuri wa kutoka upinzani kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Picha na Maktaba

Muktasari:

Akina Cannavaro wameshuka baada ya kuruhusu mabao mengi ya kufungwa, wakati Azam iking’ara kwa kufungwa mabao machache. Yanga ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ina pointi 46, imeshafungwa mabao 15 kwenye mechi 22 ilizocheza.

BEKI ya Yanga chini ya nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani ‘Vidic’, msimu uliopita ndio ilisifika kwa ubora kuliko timu nyingine za Ligi Kuu Bara hadi wakapachikwa jina la Ukuta wa Berlin. Lakini msimu huu imepigwa bao na beki ya Azam FC iliyo chini ya Aggrey Morris na Said Morad.

Akina Cannavaro wameshuka baada ya kuruhusu mabao mengi ya kufungwa, wakati Azam iking’ara kwa kufungwa mabao machache. Yanga ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ina pointi 46, imeshafungwa mabao 15 kwenye mechi 22 ilizocheza.

Idadi hiyo ni tofauti kabisa na msimu uliopita ambao walimaliza ligi yenye mechi 26 kwa kufungwa mabao 14 tu idadi ambayo sasa wameshaivuka na timu ilikuwa chini ya mabeki hao wa kati.

Msimu uliopita, Cannavaro na Yondani walisaidiwa na makipa, Ally Mustapha ‘Barthez’ na Mghana Yaw Berko anayeichezea Simba kwa sasa, mabeki wa pembeni walikuwa ni Mnyarwanda Mbuyu Twite aliyekuwa upande wa kulia na kushoto kulikuwa na David Luhende na Oscar Joshua.

Msimu huu wanacheza na mabeki wa pembeni, Mbuyu na Juma Abdul upande wa kulia, kushoto ni Oscar na Luhende wakati makipa wao ni Juma Kaseja, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Barthez ambao wanapokezana.

Azam ilimaliza ligi msimu uliopita kwa kuruhusu mabao 20 ikiwa na mabeki tofauti; Aggrey Morris, Said Morad, Erasto Nyoni na Samir Nuhu lakini mzunguko wa pili walicheza, David Mwantika, Mkenya Jockins Atudo baada ya Morad, Nyoni na Aggrey kufungiwa.

Msimu huu hadi sasa imepiga bao kwa kuruhusu mabao 14 tu ya kufungwa baada ya kucheza mechi 23, idadi ambayo ni ndogo ukifananisha na msimu uliopita.

Kocha wa Rhino, Renatus Shija, amesema: “Matokeo hayo huwa yanatokana na mfumo wa timu, huenda ni kushambulia kama wanashambulia wengi na kuzuia wachache inatokea hivyo. Inaweza kuwa kipa maana ndiyo beki wa kwanza au mabeki wenyewe kutokuwa na umakini wa kuzuia.”