Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Stellenbosch auogopa mziki wa Mpanzu

Muktasari:

  • Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Unguja, Zanzibar, Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa na kiungo mshambuliaji, Jean Charles Ahoua dakika ya 45+2.

MECHI ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Stellenbosch dhidi ya Simba itakayopigwa Aprili 27, 2025 kwenye Uwanja wa Moses Mabhida, Durban nchini Afrika Kusini, imeendelea kugusa hisia za mashabiki huku kukiwa na presha kubwa kambini kwa Stellenbosch.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Unguja, Zanzibar, Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa na kiungo mshambuliaji, Jean Charles Ahoua dakika ya 45+2.

Baada ya matokeo hayo, beki wa kushoto wa Stellenbosch, Enyinnaya Godswill, ameliambia Mwanaspoti kuwa mmoja wa wachezaji aliyekuwa msumbufu zaidi kwao kutokana na kasi na uwezo wa kubadilika ghafla ni Elie Mpanzu, winga wa Simba mwenye asili ya DR Congo ambaye anaamini anaweza kuwa kikwazo tena watakaporudiana, hivyo lazima wafanye kazi ya ziada kumdhibiti.

“Nilijipanga zaidi kukabiliana na Kibu Denis ambaye nilijua ni mbaya akiwa na mpira, lakini ukweli ni kwamba Mpanzu alitufanya tufikirie mara mbili. Ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi za hatari, kukimbia na kukokota mpira. Ni mchezaji ambaye hawezi kutabirika, tuna kazi ya kukabiliana naye tena,”  alisema.

Godswill aliyeshindwa kumaliza mchezo wa kwanza bila kuonyeshwa kadi, alipata kadi ya njano baada ya kumchezea faulo Mpanzu aliyekuwa akikokota mpira kutoka eneo la nyuma kwenda mbele.

“Mchezo ule ulikuwa mgumu. Sio kwamba tulicheza vibaya, lakini Simba walitufundisha kitu. Wanajua kucheza mechi kubwa. Tunajua kazi yetu Durban si rahisi,” aliongeza Godswill.

Simba itaingia kwenye mchezo huo wa marudiano ikiwa na faida ya ushindi nyumbani. Hata hivyo, kikosi hicho kinatambua kuwa Stellenbosch imepoteza mchezo mmoja tu nyumbani katika kampeni ya CAF mwaka huu.

Takwimu zinaonyesha Stellenbosch imefunga mabao 12 katika michezo sita ya CAF nyumbani, huku ikiruhusu matatu, yote dhidi ya RS Berkane, hali inayowafanya kuwa na rekodi nzuri. Kwa upande mwingine, Simba ikiwa ugenini ina rekodi ya kushinda mechi moja dhidi ya CS Sfaxien (1-0), imepoteza mbili dhidi ya CS Constantine (2-1) na Al Masry (2-0) huku sare zikiwa mbili dhidi ya Al Ahli Tripoli (0-0) na Bravos do Maquis (1-1).

Akizungumzia mchezo huo, kocha Fadlu alisema: “Tunajiandaa kucheza mechi ya maisha yetu. Stellenbosch ni timu ngumu lakini tumeshazoea mazingira ya presha. Tunahitaji nidhamu, umoja na umakini.”