Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brandts: Tupo tayari kuizima Simba

Kocha wa Yanga Ernest Brandts ambaye amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kuwakabili Simba. Picha na Maktaba

Muktasari:

Timu hizo zitapambana Desemba 21 mwaka huu katika mchezo maalumu wa Nani Mtani Jembe ambao umeandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na kusimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

YANGA imefanya mazoezi kwa wiki tatu sasa huku zikiwa zimebaki siku saba tu kupambana na watani zao Simba, lakini kocha wa timu hiyo, Ernest Brandts amewasifu wachezaji wake kwa kusema wameiva na wana stamina nzuri ya kumudu pambano hilo.

Timu hizo zitapambana Desemba 21 mwaka huu katika mchezo maalumu wa Nani Mtani Jembe ambao umeandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na kusimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Brandts raia wa Uholanzi aliiambia Mwanaspoti kwamba, kimsingi matayarisho ya mchezo huo yanakwenda vizuri na wachezaji wake wapo sawa kiakili na wameonyesha uwezo mkubwa katika mazoezi.

“Najua tunaenda kucheza na Simba ndani ya siku chache zijazo, jambo la msingi ni kwamba nashukuru tunaendelea vizuri na mazoezi yetu hivyo timu ipo tayari kwa mchezo wowote ulio mbele yetu,” alisema Brandts aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi.

Kocha huyo alisema anajua kinachotakiwa kufanywa kabla ya kucheza mchezo kama huo, ndiyo maana anawafanyisha mazoezi ya kasi uwanjani wachezaji wake na wakati mwingine huwapeleka ‘gym’ kuwaongezea stamina.

“Wachezaji wote (wa Yanga) wanajua jambo la kufanya katika mechi kubwa kama hiyo, lakini naamini kwa mazoezi tuliyofanya watafanya kitu kizuri katika mchezo huo,” alisema Brandts.

Yanga inafanya mazoezi bila ya wachezaji wake waliopo katika kikosi cha Kilimanjaro Stars waliokuwa wakishiriki Kombe la Chalenji huko Kenya na Said Bahanuzi aliyeenda kufanya majaribio Malaysia.

Wachezaji wa Yanga waliopo Kilimanjaro Stars ni pamoja na Deo Munishi ‘Dida’, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Athumani Idd ‘Chuji’, Hassan Dilunga (amesajiliwa kutoka Ruvu Shooting) na Mrisho Ngassa mabao watajiunga na wenzao Jumatatu. Hamis Kiiza yupo kwao Uganda kwa ruhusa maalumu baada ya kufiwa na baba yake mlezi.

Wachezaji wanaohudhuria mazoezi ya timu hiyo ni Ali Mustapha ‘Barthez’, Juma Kaseja, Yusuf Abdul, Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Nizar Khalfan, Salum Telela, Hussein Javu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Jerry Tegete, Oscar Joshua, Bakari Masoud, Ibrahim Job, Simon Msuva, Hamis Thabit, Rajab Zahir, Shaaban Kondo, Abdallah Mguhi, Didier Kavumbagu na Reliants Lusajo.

Hii itakuwa mechi ya tatu ya Simba na Yanga kukutana mwaka huu ambapo katika mechi ya msimu uliopita uliozikutanisha timu hizo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, kisha timu hizo zikatoka sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi.

Hata hivyo Simba inahitaji kufanya kazi ya ziada kwani ina kikosi chenye wachezaji wengi chipukizi huku ikiwa na kocha mpya Zdravko Logarusic kutoka Croatia ambaye amesaini mkataba wa miezi sita tu kuifundisha timu hiyo.