Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ceasiaa Queens yalia na ratiba WPL

Ceaseaa Pict

Muktasari:

  • Awali, mechi hiyo ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa TFF Kigamboni, Machi 12 lakini imesogezwa siku nne mbele huku sababu za kufanya hivyo zikiwa hazijulikani.

KOCHA wa Ceasiaa, Ezekiel Chobanka amesema mvurugano wa ratiba umeathiri kiasi kikubwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Mlandizi Queens.

Awali, mechi hiyo ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa TFF Kigamboni, Machi 12 lakini imesogezwa siku nne mbele huku sababu za kufanya hivyo zikiwa hazijulikani.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chobanka alisema kama timu wanapambana kupata mechi angalau moja ya kirafiki ili kurejesha ufiti wa wachezaji.

“Kwa sisi ambao tuko mikoani hasa Iringa hakuna timu nyingine zinazoshiriki Ligi, tumekaa zaidi ya mwezi hamna mechi, napambana kuja mapema Dar es Salaam kupata mechi za kirafiki,” alisema Chobanka.

“Kuna haja TFF kuangalia namna nzuri ya kuweka mpangilio wa ratiba ili kusaidia na timu za mikoani ambazo zinatumia gharama kubwa za usafiri kufika Dar.”

Hii ni mara ya pili timu hizo zinakutana msimu huu, awali Ceasiaa ilishinda mabao 5-0.