Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania Prisons itaishusha KenGold Sokoine leo?

PRISONS Pict

Muktasari:

  • Kitakwimu kama KenGold itakubali kupoteza mchezo huo huenda ikawa imeshuka daraja kwani hesabu za vidole zitakazosalia si rafiki kwao.

KATIKA uwanja wa Sokoine, Mbeya  Kengold FC ambao wanaburuza mkia wakiwa na pointi 16 watakuwa na mtihani mgumu dhidi ya Tanzania Prisons, walioko nafasi moja juu yao wakiwa na pointi 21.

Kitakwimu kama KenGold itakubali kupoteza mchezo huo huenda ikawa imeshuka daraja kwani hesabu za vidole zitakazosalia si rafiki kwao.

Kumbukumbu za misimu mitatu nyuma zinaonyesha kwamba timu yoyote iliyoshindwa kufikisha pointi 30 ilishuka moja kwa moja. KenGold wasipoishinda Prisons hawawezi kufikisha pointi 30.

Baada ya mechi hii KenGold itabakiwa na michezo minne dhidi ya Coastal Union na Namungo ugenini na Pamba na Simba nyumbani.

Mchezo huo unakuja huku Kengold ikiwa kwenye hali mbaya zaidi baada ya kuchapwa mechi mbili mfululizo dhidi ya Azam FC (2-0) na  Dodoma Jiji (3-0), hali iliyowaweka kwenye presha kubwa ya matokeo.

Prisons na wenyewe hawako salama kimahesabu kwani wanalazimika kupata pointi muhimu ingawa bado wanapumua kuliko majirani zao. 

Kocha wa KenGold, Omary Kapilima, anakabiliwa na presha ya kusaka ushindi wa lazima nyumbani kwani wapinzani wao Tanzania Prisons wanakuja na morali ya ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya Kagera Sugar, huku kocha wao Amani Josiah akikiri kuwa wanakutana na timu wanayoifahamu vyema.

“Ni mechi ngumu sana, lakini tumejiandaa. Tunahitaji pointi hizi kama wao wanavyozihitaji. Tunajua udhaifu wao, tunajua nguvu zao. Tutapambana hadi dakika ya mwisho,” alisema Josiah.

Kwa upande wa KenGold, wanabeba matumaini yao kwa Seleman Bwenzi ambaye tayari amefunga mabao matano, sambamba na Obrey Chirwa ambaye alijiunga katika dirisha dogo na kufunga mabao mawili hadi sasa.

Kwa Tanzania Prisons, hakuna mfungaji aliyevuka mabao manne msimu huu, lakini wakiwa na wachezaji wenye uzoefu kama Haruna Chanongo (mabao 3), wanaamini mbinu na nidhamu ya uchezaji vinaweza kuwapa matokeo.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Prisons waliibuka na ushindi wa bao 1-0, hivyo Kengold wanaingia wakitafuta kulipiza kisasi cha matokeo hayo.


DODOMA JIJI VS KAGERA SUGAR

Wakati huo huo, Uwanja wa Jamhuri Dodoma utakuwa mwenyeji wa pambano kati ya wenyeji  Dodoma Jiji FC, waliopo nafasi ya saba na pointi 31, dhidi ya Kagera Sugar walioko nafasi ya 14 wakiwa na pointi 22.

Dodoma Jiji chini ya kocha Meck Mexime wamekuwa kwenye mwelekeo mzuri, hasa baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kengold, na wanahitaji pointi tatu nyingine leo ili kusogea karibu na timu zinazowania nafasi za juu za msimamo.

Kwa upande wa Kagera Sugar, licha ya kupoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Prisons, wana rekodi ya kuvuna pointi 6 kati ya 9 zilizopita, hali inayowapa matumaini ya kufanya vizuri leo na kuifikia Coastal Union walioko nafasi ya 13 kwa pointi 25.

Kagera Sugar chini ya kocha Juma Kaseja wanaendelea kupambana kuhakikisha msimu huu hauwi wa huzuni. Mchezo huu ni muhimu sana kwa mustakabali wao.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza kati ya timu hizi, Kagera Sugar waliibuka na ushindi wa mabao 2-1, jambo ambalo linawapa motisha ya kuendeleza ubabe mbele ya Dodoma Jiji