Chama afiwa na mkewe Zambia

Taarifa za kusikitisha ni kwamba mke wake kiungo wa Simba Clatous Chama amefariki leo nchini Zambia.
Taarifa zilizothibitishwa na kocha wa zamani wa Yanga na raia wa Zambia, Noel Mwandila ni kwamba mke wa Chama aitwaye Mercy amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Inaelezwa Mercy aliugua na kukimbizwa Hospitali ya Kitwe siku chache zilizopita lakini wakati akipatiwa vipimo alipoteza maisha.
"Nikweli huku Zambia kuna hizo taarifa mbaya za Chama kufiwa na mkewe,ameugua kwa siku chache sana ni taariga mbaya kwa kila mmoja sio tu huko Tanzania hata huku Zambia," amesema Mwandila ambaye sasa ni kocha msaidizi wa Zesco ya Zambia.
Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amethibitisha taarifa hizo na kusema taarifa wamezipata mchana wa leo na msiba upo Lusaka, Zambia.
"Baada ya mechi kumalizika benchi la ufundi na wachezaji watakaa kikao kujua nini watafanya," amesema Matola