Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe, Bellingham tumbo joto La Liga

Coastal Pict
Coastal Pict

Muktasari:

  • Mbappe na Bellingham walichukua hatua ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii wakikubali kuwa wanahitaji kuboresha viwango vyao kabla ya mchezo wao wa Arsenal.

MADRID, HISPANIA: MASTAA wa Real Madrid, Kylian Mbappe na Jude Bellingham, walikiri kuwa hawakuwa bora vya kutosha katika kipigo cha kushangaza nyumbani kwao dhidi ya Valencia Jumamosi na wanajipanga wao kama wachezaji kuhakikisha wanabadilika kabla ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal.

Mbappe na Bellingham walichukua hatua ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii wakikubali kuwa wanahitaji kuboresha viwango vyao kabla ya mchezo wao wa Arsenal.

Madrid ilipata kipigo cha dakika za 'jiooni' cha mabao 2-1 kutoka kwa Valencia, na kuachwa pointi nne nyuma ya vinara wa La Liga na mahasimu wao Barcelona.

Kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram, Mbappe alisema: "Siku mbaya kwetu. Tumekazia macho yote Jumanne." 

Kwa upande wa Bellingham alisema: "Hatujaonyesha kiwango bora. Lazima tubadilike kuelekea mchezo wetu wa Jumanne."

Arsenal na Madrid zitakuwa zinakutana katika nyakati ngumu kwa timu zote kwani mbali ya Madrid kutoka kupoteza, Arsenal pia iliambuliwa sare dhidi ya Everton.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana tangu mwaka 2006 ambapo mara ya mwisho Arsenal ilishinda bao 1-0.