Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eto’o, Sakho katika kisa cha Santos wa Arsenal

Muktasari:

  • Mashabiki wa Arsenal walichukia sana, hasa ukizingatia Mdachi huyo tayari alikuwa amewafunga bao katika dakika ya tatu tu ya mchezo. Kipindi cha pili, Santos hakurudi tena uwanjani na huo ukawa mwisho wake Emirates kabla ya kurudishwa kwao Brazil.

LONDON, ENGLAND

KAMA kuna kitu ambacho Mbrazili, Andre Santos, anajuta kukifanya kwenye zama zake alizokuwa kwenye kikosi cha Arsenal ni kubadilishana jezi na Robin van Persie wakati wa mapumziko, timu yake ilipomenyana na Manchester United kwenye Ligi Kuu England uwanjani Old Trafford msimu uliopita.

Mashabiki wa Arsenal walichukia sana, hasa ukizingatia Mdachi huyo tayari alikuwa amewafunga bao katika dakika ya tatu tu ya mchezo. Kipindi cha pili, Santos hakurudi tena uwanjani na huo ukawa mwisho wake Emirates kabla ya kurudishwa kwao Brazil.

Kilichoichukiza Arsenal ni Santos kubadilishana jezi wakati wa mapumziko. Lakini, pia ni mtu aliyebadilishana naye. Van Persie, ametoka kawafunga na kisha anampa jezi yao, hiyo iliwakera sana mashabiki wa timu hiyo.

Binafsi, sidhani kama Santos alikosea. Mbrazili huyo alitambua wazi kwamba asingeweza kurudi tena kipindi cha pili na jezi ya Van Persie, aliyekuwa nahodha wake Emirates alikuwa akiitaka, angefanyaje sasa zaidi ya kuichukua mapema?

Arsene Wenger na mashabiki wake walimshambulia sana kwa kitendo hicho. Arsenal hawakuchukia kwa sababu Santos amegawa jezi wakati wa mapumziko, bali wamechukizwa na mtu aliyebadilishana naye jezi hiyo.

Juzi Jumapili kulikuwa na tukio kama hilo.  Kwenye mchezo kati ya Chelsea na Liverpool kuna wachezaji wanne walibadilishana jezi wakati wa mapumziko.

Beki wa Liverpool, Mamadou Sakho alibadilishana jezi na Samuel Eto’o, wakati Coutinho alibadilishana na Oscar.

Kitendo hicho ni kama alichowahi kufanya Santos na Van Persie kwenye Ligi Kuu.

Rodgers achukia

Baada ya tukio la Sakho kumpa jezi Eto’o limemkera pia kocha Brendan, licha ya mpinzani wake Jose Mourinho kukaa kimya juu ya jambo hilo baada ya kuona hakuna sababu ya kulitolea macho.

Mourinho haoni kama wachezaji wake wamefanya dhambi kwenye hilo.

Arsenal wanaheshimu jezi

Utamaduni wa Arsenal unaonekana kuheshimu sana jezi zao. Mfano mzuri wa jambo hilo ni kisa cha kiungo Flamini na jezi ya mikono mifupi. Kwa msimu huu wanaozuia kuvaa jezi za mikono mifupi. Flamini anateseka na utamaduni huo wa kumlazimisha avae jezi yenye mikono mirefu.

Kwa sababu jezi za Arsenal kwa msimu huu ni za mikono mirefu, jambo hilo limemfanya Flamini mara kadha kuzikata kwa mkasi kupunguza mikono kitu kilichomtia kwenye malumbano na kocha wake.

Flamini amekubali masharti ya Wenger, lakini bado uwanjani anaonekana akiwa amekunja jezi yake na kuonekana kama ya mikono mifupi.

Lakini, turudi kwenye mjadala wetu kuhusu wachezaji kubadilishana jezi. Ni wakati gani mzuri na sahihi, baada ya kipindi cha kwanza au mechi inapomalizika?

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, kati ya Chelsea na Liverpool baada ya dakika 45 za kwanza na wachezaji wakiwa wanaelekea vyumbani baadhi ya wachezaji walionekana kubadilishana jezi. Wamefanya hivyo bila ya woga wowote wa kwamba wangeandamwa na mashabiki wao kama wale wa Arsenal walivyomfanyia Santos.

Baada ya mwamuzi Howard Webb kupuliza kipyenga wakati wa mapumziko, beki wa Liverpool, Mfaransa Mamadou Sakho alimpa jezi Eto’o na kisha yeye akachukua ya kwake. Kumbuka Eto’o ndiye aliyewafunga bao la pili la ushindi wa kwa Chelsea.

Coutinho na Mbrazili mwenzake Oscar nao wakafanya hiyo.

Rodgers ameng’ata kwa Sakho, lakini haifahamiki kama atampa adhabu kwa sababu michezo ni uungwana na katika dunia ya sasa suala la kubadilishana jezi ni utamaduni wa kawaida tu.

Wachezaji wa Raja Casablanca waligombea viatu vya Mbrazili Ronaldinho baada ya kucheza dhidi yake kwenye mechi ya Klabu Bingwa ya Dunia wiki iliyopita kule Morocco. Ronaldinho alibaki anacheka tu na kila mtu alielewa kwanini wachezaji hao walitaka viatu vya staa huyo. Kilichowasukuma Raja ndicho kilichomsukuma Santos kwa Van Persie, kwa sababu ndiye mchezaji anayemhusudu uwanjani, ndiye shujaa wake.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Robinho wa AC Milan alibadilishana jezi na Mbrazili mwenzake, Neymar wa Barcelona, wakati timu zao zilipomenyana. Neymar alilifanya hilo kipindi cha mapumziko tu kwa sababu Robinho ndiye mchezaji aliyekuwa akimtazama na siku zote anacheza akitamani kuwa kama yeye.

Kucheza dhidi yake ya mchezaji unayemhusudu ni sehemu muhimu kwa wachezaji kuweka kumbukumbu zao na hivyo kupeana jezi ni jambo linaloonekana lina maana kwao.