Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fadlu ashtukia mchongo, apanga upya silaha zake

Muktasari:

  • Kwa sasa Simba inacheza mechi za viporo za Ligi Kuu Bara kabla ya kwenda kucheza mechi ya fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane.

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davis amesema anafanya mabadiliko ya kikosi chake kutokana na ugumu wa ratiba na ataendelea kufanya hivyo kwa kuwapa mapumziko ya kutosha nyota wake ili kufikia malengo.

Kwa sasa Simba inacheza mechi za viporo za Ligi Kuu Bara kabla ya kwenda kucheza mechi ya fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fadlu amesema ratiba upande wao ni ngumu lakini anawapongeza wachezaji wake kwa kufuata maelekezo anayowapa na kuipambania timu kupata matokeo mazuri huku akiamini wataendelea kufanya hivyo na kufikia malengo ya kutwaa mataji.

"Kucheza mechi nne ndani ya siku kumi sio jambo rahisi, tuna siku mbili katikati ya mechi ya Pamba na KMC, sio rahisi kuingia na kikosi kilekile, nitafanya mabadiliko bila kufuata mfumo lakini naamimi tutapata matokeo mazuri,” amesema na kuongeza.

"Jumanne tutafanya tathmini, tutapokea ripoti ya madaktari na kufanya 'recovery' ili tupate kikosi cha kuikabili Pamba, sio rahisi lakini nina imani kubwa na wachezaji wangu watafanya vizuri.”

Kuelekea mechi mbili zinazofuata, Fadlu amesema muhimu kwao ni pointi tatu na wanalazimika kubadili mtindo wa uchezaji katika eneo lao la mbele kwa kuchezesha wachezaji bila kuzingatia nafasi lengo ni kuona wanatoa nafasi kwa kila mchezaji na kuwapumzisha wengine.

"Sasa tutakuwa tukicheza kwa kuitanua safu ya ulinzi ya wapinzani, ili kutengeneza nafasi katikati na kutumia zaidi wachezaji wenye kasi kutokea pembeni, sio wakati wa kuzingatia mifumo, ni mbinu tu.

"Haijalishi tunacheza na washambuliaji asili mmoja au wawili, au tunacheza na mshambuliaji wa uongo (false 9), muhimu kwetu ni kusaka alama tatu,” amesema Fadlu.

Simba tayari imekusanya pointi sita kwenye viporo viwili walivyocheza hadi sasa wakianza na Mashujaa kwa kuitandika mabao 2-1, kisha wakaifunga JKT Tanzania bao 1-0, zimebaki mechi mbili za viporo dhidi ya Pamba Jiji (Mei 8) na KMC (Mei 11), kabla ya Mei 17 kukabiliana na RS Berkane.