Gets Program inazitaka pointi tisa WPL

Muktasari:
- Gets iko nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi na ilikuwa miongoni mwa timu mbili zilizoanza vibaya kwenye mechi 15 imeshinda mbili, sare nne na kupoteza tisa ikiruhusu mabao 39.
KATIKA kuhakikisha inasalia Ligi Kuu, Gets Program imeanza mipango ya kuzisaka pointi tisa zilizosalia, ingawa kocha wa timu hiyo, Aristides Ngowi amesema haitakuwa kazi rahisi.
Gets iko nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi na ilikuwa miongoni mwa timu mbili zilizoanza vibaya kwenye mechi 15 imeshinda mbili, sare nne na kupoteza tisa ikiruhusu mabao 39.
Akizungumzia juu ya mipango hiyo, kocha Ngowi alisema haitakuwa rahisi lakini wakishinda mechi hizo itawabakisha Ligi Kuu.
Aliongeza pointi tisa ni muhimu kwao za kufa na kupona ili kulipia mwanzo mbaya waliouanza.
"Ligi ilipofikia kuna vita ya ubingwa na sisi ambao tunawania nafasi za kubaki, tutapambana kwa kila hali kubaki hatutaki kurudi Ligi Daraja la Kwanza," alisema na kuongeza;
"Vijana wamekuwa na muendelezo wa kile nilichokuwa nawaelekeza, Gets tuna wachezaji wengi wadogo ambao hawana uzoefu, tunafikiri msimu ujao unaweza kuwa bora kama wakizoea haraka lakini kwa walipofika wanajitahidi sana."