Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kina Samatta wanyang’anywa simu Stars

Muktasari:

  • Nooij alifanya hivyo ili wachezaji hao watulize akili na kufikiria mchezo huo wa raundi ya kwanza wa kufuzu fainali za Afrika (Afcon). Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bao pekee la Stars lilifungwa na John Bocco katika dakika ya 13 baada ya kupokea krosi ya Thomas Ulimwengu na kupiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni.a

KOCHA wa Taifa Stars,Mart Nooij ameanza kazi na staili yake. Bosi huyo aliwapokonya simu wachezaji wote siku moja kabla ya mchezo wa jana Jumapili dhidi ya Zimbabwe ambapo Stars ilishinda bao 1-0.

Nooij alifanya hivyo ili wachezaji hao watulize akili na kufikiria mchezo huo wa raundi ya kwanza wa kufuzu fainali za Afrika (Afcon). Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bao pekee la Stars lilifungwa na John Bocco katika dakika ya 13 baada ya kupokea krosi ya Thomas Ulimwengu na kupiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Dakika ya 17, Ulimwengu aliipangua ngome ya Zimbabwe na kupiga krosi ambayo iliokolewa na kipa wa Zimbabwe George Chigova, ambapo Zimbabwe nao walijibu mashambulizi dakika ya 23 kwa kulishambulia lango la Stars lakini kipa Deo Munishi ‘Dida’ alikuwa imara kuokoa hatari.

Mwamuzi wa mchezo huo Joseph Lamptey kutoka Ghana alitoa kadi ya njano dakika ya 20 kwa Milton Nkube aliyemchezea rafu Mbwana Samatta, huku dakika ya 25 Zimbabwe walipata faulo iliyopigwa na Nkube lakini alipaisha mpira juu.

Dakika ya 31, Oscar Joshua nusura ajifunge baada ya kumrudishia mpira Dida huku Wazimbabwe wakionekana kushambulia zaidi langoni mwa Taifa Stars ingawa dakika ya 40 Samatta aliangushwa katika eneo la hatari lakini hawakuweza kupata penalti.

Katika kipindi cha kwanza Ulimwengu alichezewa rafu na kusababisha kupata maumivu hivyo kutolewa nje kwa machela huku safu ya ulinzi ya Zimbabwe ikionekana kuwa imara zaidi kwani mbinu za Samatta, Ulimwengu, Mrisho Ngassa na Bocco zilidhibitiwa kabla ya kufika langoni.

Dakika ya 46, Zimbabwe walifanya shambulizi langoni mwa Stars lakini shuti kali lililopigwa nje ya 18 na   Manachi liliokolewa na Dida. Ulimwengu alijibu shambulizi dakika ya 47 akitoa krosi kwa Bocco ambaye alipaisha juu ya goli ambapo dakika ya 50 Ulimwengu alipewa kadi ya njano kwa kujiangusha makusudi.

Samatta alipiga mashuti makali dakika ya 52 na 57 lakini yaliokolewa na kipa wa Zimbabwe huku mchezaji wa Zimbabwe Manachi naye akiwa amebaki na Dida golini dakika ya 56 alipiga mpira na kupaa juu.

Mchezaji wa Zimbabwe, Steven Almenda naye alipewa kadi ya njano.

Kocha wa  Zimbabwe, Ian Gorowa alifanya mabadiliko katika dakika ya 58 akimtoa Peter Moyo na kumwingiza Kudakwashe Mushuru, mabadiliko yalifanyika tena kwa kumtoa Tendai Ndoro na kumwingiza Marshal Mudehwe.

Naye kocha wa Stars, Mart Nooij alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Ngassa nafasi yake ilichukuliwa na Ramadhani Chanongo, Frank Domayo na kumwingiza Amri Kiemba, Bocco nafasi yake ilichukuliwa na Hamis Mcha.

Mwamuzi aliendelea kutoa kadi za njano ambapo dakika ya 88, mchezaji wa Zimbabwe Eric Chipeta alipewa kadi kwa kumchezea rafu Ulimwengu.

Kocha wa Zimbabwe, Gorowa, ameipongeza Stars kwa ushindi wa bao hilo na kudai kuwa wanakwenda kujipanga na wataitumia vizuri nafasi ya nyumbani ambayo itakuwa na faida kwao.

Naye Nooij amewapongeza wachezaji wake lakini amedai kuwa watahakikisha wanalinda ushindi wa bao hilo katika mechi ya marudiano huku akidai kuwa wana faida ya bao la ugenini.

Taifa Stars: Dida, Shomari Kapombe, Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Bocco, Samatta na Ulimwengu.