Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiwango cha Karabaka chazua vikao

KARABAKA Pict

Muktasari:

  • Januari  23, 2025 Karabaka alijiunga na Simba  akitokea  JKU SC ya Zanzibar, dirisha dogo la msimu uliyopita akiwa ameifungia mabao mawili na asisti mbili,  klabu hiyo ilimtoa kwa mkopo kwenda kuichezea Namungo FC.

KUNA taarifa za ndani za Simba kufanya mazungumzo na winga anayecheza JKT Tanzania kwa mkopo, Salehe Karabaka baada ya kuonyesha kiwango cha juu kulichoivutia klabu hiyo na kuhitaji huduma yake kwa mara nyingine tena.

Januari  23, 2025 Karabaka alijiunga na Simba  akitokea  JKU SC ya Zanzibar, dirisha dogo la msimu uliyopita akiwa ameifungia mabao mawili na asisti mbili,  klabu hiyo ilimtoa kwa mkopo kwenda kuichezea Namungo FC.

Karabaka alitolewa kwa mkopo kwa sababu alikuwa na nafasi finyu Simba na washindani wake walikuwa ni Kibu Denis aliyemaliza msimu huo akiwa na mabao manne, asisti nne, Elie Mpanzu mabao manne, asisti tano, Joshua Mutale hakuwa na bao bali asisti mbili na klabu hiyo ilimuondoa katika mpango wa msimu huu haikuridhishwa na kiwango chake.

KARA 01

Wakati anakwenda kujiunga Namungo, kocha Juma Mgunda amesema:”Karabaka ni mchezaji mzuri, isipokuwa amekosa nafasi Simba mbele ya wachezaji wazoefu lakini akicheza mara kwa mara kipaji chake kitaonekana kwa ukubwa.”

Msimu huu bado anacheza kwa mkopo JKT Tanzania, huku tetesi zikisema mkataba wake na Simba unaishia baada ya ligi kumalizika pamoja na hilo bado Wanamsimbazi wanaonyesha kuhitaji huduma yake kwa ajili ya msimu ujao kama chanzo kinavyoeleza kuwepo kwa mazungumzo baina ya mchezaji na uongozi wa klabu hiyo.

Chanzo hicho kilisema:”Uongozi wa Simba unakaa kujadili kuona jinsi ya kumuongezea Karabaka mkataba kwa kuwa amekuwa akionyesha kiwango bora. Huyu anapewa nafasi kama mchezaji mzawa na baada ya kutolewa kwa mkopo ameendelea kupambana na kuonyesha alikosa nafasi, lakini alipopewa nafasi JKT kaonyesha uwezo wake mzuri.”

KARA 02

Alipotafutwa Karabaka ambaye msimu huu amefunga mabao nane kwenye ligi amesema:”Sijui chochote kuhusiana na hilo, ninachokizingatia ni kufanya kazi ninayoelekezwa na kocha Ahmad Ally na namshukuru kwa kunipa nafasi ya kucheza.”

Kocha Ally amesema:”Karabaka ni mchezaji mzuri kijana, bado ana muda wa kuzipambania ndoto zake, kama kocha nafurahia kuona wachezaji ninaowafundisha wanatajwa miongoni mwa walio bora katika Ligi Kuu.”

Staa wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Zamoyoni Mogella amesema:”Nitolee mfano wa  Nickson Kibabage wakati anajiunga Simba ilionekana si mchezaji anayetakiwa katika mapinduzi ya kikosi cha kunyakua mataji, akaamua kujituma na kuonyesha kiwango cha umuhimu wa yeye kuwepo kikosi cha kwanza, vivyo hivyo kwa Karabaka akifanikiwa kurejea Simba asijichukulie kama chaguo la pili.”