Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha JKT Tanzania awaondolea mzigo Bocco, Songo

BOCCO Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo ambayo inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikikusanya pointi 30, imeshuka dimbani mara 23, imeshinda 7, sare 9 na kupoteza 7, ina mabao ya kufunga 18 na kuruhusu 17, jambo ambalo kocha huyo analiona lina uwiano mzuri na wachezaji wanacheza kitimu.

KOCHA wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amesema anatengeneza timu ambayo haitakuwa mzigo kwa baadhi ya wachezaji, badala yake anahitaji kila anayekuwa uwanjani ajue yupo kwa ajili ya kupambania pointi tatu.

Alisema anatambua washambuliaji kama John Bocco mwenye mabao mawili na Edward Songo aliyefunga matatu hiyo ni kazi yao, lakini hataki kuwapa presha kutimiza majukumu yao zaidi ya kuitengeneza timu ambayo mchezaji yeyote anafunga kama ilivyo kwa beki wa kikosi hicho, Wilson Nangu mwenye mabao mawili Ligi Kuu na moja Kombe la FA.

“Kuwapa presha wachezaji hakuwasaidii badala yake utazidi kuwaondoa katika mstari, ukiangalia msimamo wa ufungaji katika timu yangu unatafsiri kama timu haifungi mabao mengi basi isifungwe,” alisema kocha huyo na kuongeza:

“Mapumziko haya ya ligi yametusaidia kufanya tathimini kama kuna sehemu ilikuwa na upungufu tujue tukabiliane nayo vipi, tuliyofanya kwa ubora tuongezee zaidi, tutacheza mechi mbili za kirafiki ambazo zitazidi kutupa picha kamili ya kipi tukitarajie kukifanya katika mechi saba zilizosalia kufunga msimu huu.”

Timu hiyo ambayo inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikikusanya pointi 30, imeshuka dimbani mara 23, imeshinda 7, sare 9 na kupoteza 7, ina mabao ya kufunga 18 na kuruhusu 17, jambo ambalo kocha huyo analiona lina uwiano mzuri na wachezaji wanacheza kitimu.