Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Villa: Pasi za Oloya zinafaa Yanga

Muktasari:

  • Tatizo nililoliona kwa Yanga hawana mpikaji wa mabao (play maker) kama watampata mtu kama Moses Oloya mambo yatakwisha.

KOCHA wa Sports Club Villa ya Uganda, Steven Bugere amenyanyua mikono juu na kusema Yanga ni babu kubwa na amesisitiza, Moses Oloya anafaa kukichezea kikosi cha Jangwani na si Simba.

Pia ameipamba zaidi beki ya kati ya Yanga iliyoanza walipocheza dhidi yao juzi Jumapili; Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani kabla ya kuingia, Rajab Zahir kipindi cha pili.

SC Villa ilicheza mechi za kirafiki dhidi ya Simba Jumamosi iliyopita wakafungwa mabao 4-1 sawa na walivyofungwa na Yanga 4-1 siku iliyofuata, mechi zote kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bugere alisema: “Aisee Yanga ni kiboko, unajua kuna vitu vingi nimegundua kutoka kwao.”

“Wanacheza kwa nguvu wanalazimisha, wana kasi, lakini pia wana akili kwa kichwa. Unajua kuna mtindo fulani tuliwachezea Simba kipindi cha kwanza mechi walikubali tukatoka 1-1 kabla ya kipindi cha pili kutufunga mabao mengine ambayo yalitokana na makosa mengine ya kiufundi,” alisema kocha huyo bila kufafanua mtindo huo.

“Mtindo uleule niliijaribu kwa Yanga Jumapili, lakini wale jamaa wana akili ya mpira wakagundua, hatukufanya kitu kibaya, wakatufunga 3-1 kabla ya kipindi cha kwanza.

“Kipindi cha pili walipoingia wengine kasi yao ilipungua lakini nafikiri walijaribu kuwapa nafasi wachezaji wengine kujaribu na sisi tulirudi tumejipanga tukamaliza 4-1.

“Tatizo nililoliona kwa Yanga hawana mpikaji wa mabao (play maker) kama watampata mtu kama Moses Oloya mambo yatakwisha.

“Uganda nzima hakuna mchezaji wa kupika mabao kama Oloya na hilo hakuna atakayenibishia kwa sababu nimecheza mpira na naujua.

“Oloya utampenda acheze kiungo mshambuliaji awachezeshe mipira ya mwisho washambuliaji na kama itakuwa naye, itakuwa mfano wa kuigwa kwenye ukanda huu kwa sababu washambuliaji wao ni wazuri lakini wanakosa mtu wa kuwapikia mabao tu.

“Simba wazuri na wamekitengeneza kikosi chao, lakini bado watoto hawana mbinu nyingi,” alisisitiza Bugere.

Alipoulizwa, Oloya anafaa kuichezea timu gani kati ya Simba au Yanga, Bugere alisema: “Kwa hizi timu za Simba na Yanga, Oloya anafaa awachezee hawa Yanga tu.”

Katika hatua nyingine, Bugere amesifu zaidi safu ya beki ya kati iliyoanza walipocheza, Yondani na Cannavaro.

Katika mchezo huo, Yanga ilitumia mfumo wa 4-3-3 kwa kuwaanzisha, Ally Mustapha ‘Barthez’, beki wa kulia ilichezwa na Juma Abdul na David Luhende alicheza kushoto, mabeki wa kati ni Cannavaro na Yondani wakati kiungo ilichezwa na Athuman Idd ‘Chuji’, Haruna Niyonzima na Salum Telela.

Watatu wa mbele walicheza, Mrisho Ngassa ‘Anko’, Jerry Tegete na Mrundi Didier Kavumbagu.

Kipindi cha pili kocha, Ernie Brandts aliwatoa, Yondani, Tegete, Luhende, Chuji na Niyonzima na nafasi zao zilichukuliwa na Said Bahanuzi, Hussein Javu, Oscar Joshua, Bakari Masoud na Zahir.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Ngassa, Cannavaro, Kavumbagu na Niyonzima.