Kumbe Neymar ana mshahara mkubwa hivi

Muktasari:
- Gazeti la Les Parisiens limedai kwamba Neymar lazima awahi, aheshimu waandishi wa habari na asicheze kamari katika michuano yote ambayo PSG inashiriki. Yote haya yapo katika mkataba wake wa sasa na lazima ayatimiza.
PARIS, UFARANSA.IMEBAINIKA kwamba kumbe staa wa PSG, Neymar analipwa mshahara kubwa kuliko ule ambao tunaujua. Wadakuzi wa mambo wamepekua na kugundua kuwa Neymar analipwa mshahara wa Pauni 900,000 kwa wiki.
PSG ambao walivunja rekodi ya uhamisho ya dunia mwaka jana kwa kutoa kiasi cha pauni 198 milioni kumnunua Neymar kutoka Barcelona inadaiwa pia kuwa waliwalipa pesa, mawakala wake, baba yake, na klabu yake ya kwanza Santos kama sehemu ya kumnasa Neymar.
Kuna vipengele vya ajabu katika mkataba wa Neymar kama vile mchezaji huyo kulazimika kuwapungia mikono mashabiki wa PSG pindi mechi yoyote inapomalizia. Endapo hatafanya hivyo kuna kiasi cha pesa atakatwa.
Gazeti la Les Parisiens limedai kwamba Neymar lazima awahi, aheshimu waandishi wa habari na asicheze kamari katika michuano yote ambayo PSG inashiriki. Yote haya yapo katika mkataba wake wa sasa na lazima ayatimiza.
Kwa dau hilo analolipwa Neymar kwa wiki linamfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani kwa sasa kuliko wote, ingawa awali ilikuwa inadhaniwa kwamba mastaa wa Juventus na Barcelona, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi walikuwa juu yake.