Kunihira, Mukandasyenga kwenye vita ya kiatu

Muktasari:
- Kunihira ambaye anaitumikia Ceasiaa amefunga mabao manane huku Mukandaysenga akiwa na mabao saba kwenye mechi sita alizocheza.
WASHAMBULIAJI Magret Kunihira wa Ceasiaa Queens na Jeaninne Mukandayyenga wanaingia kwenye vita ya ufungaji ambayo hadi sasa inaoenakana kuwania na Stumai Abdallah wa JKT Queens mwenye mabao 26 na Jentrix Shikangwa wa Simba mwenye 19.
Kunihira ambaye anaitumikia Ceasiaa amefunga mabao manane huku Mukandaysenga akiwa na mabao saba kwenye mechi sita alizocheza.
Hii ni mara ya kwanza kwa nyota hao wa kigeni kuingia kwenye 10 bora za watupiaji na mabao yao yamekuwa na msaada kwenye timu wanazozichezea.
Kunihira amecheza mechi zote 14 akifunga mabao hayo ambayo yameisaidia Ceasiaa kusalia nafasi ya tano kwenye msimamo na pointi 16.
Mukandaysenga amecheza mechi sita akiingia kikosini hapo dirisha dogo na tayari amefunga mabao saba akiingia kwenye vita na Stumai na Shikangwa.
Kama nyota hao wataendelea kufunga kwenye mechi nne zilizosalia huenda wakamaliza kwenye tatu bora.