Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeshi ya Yanga na Simba yaenda mafichoni

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’, alipanda ndege jana Jumatano asubuhi akitangulia Zanzibar huku akiwaachia timu wasaidizi wake, Selemani Matola na Idd Pazzi (Kocha wa Makipa) waliondoka na kikosi kwa boti, lakini imeelezwa timu nzima itarejea Dar kwa ndege kuhofia kuchoka.

Muktasari:

Simba imetangulia kuingia kambini, kama ilivyo kawaida yao imekimbilia Zanzibar ambako huweka kambi ya kujiandaa kuivaa Yanga na imeondoka Dar es Salaam ikiwa na msafara wa nyota wake 18.

AZAM FC imeshatangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ndiyo bingwa mpya hakuna ubishi. Imefanya hivyo ikiwa na mechi moja mkononi itakayopigwa Jumamosi. Lakini hilo halibadilishi ule utamu wa mechi ya watani, Simba na Yanga, itakayopigwa siku hiyo pia.

Angalau Yanga ina uhakika wa kushika nafasi ya pili baada ya kujikusanyia pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine zilizo chini yake na hata Simba ambayo itaingia katika mchezo huo ikisaka heshima tu kwani hata ikiibuka na ushindi wa mabao 10-0 haitaweza kupanda kokote wakiwa katika nafasi yao ya nne wakiwa na pointi 37.

Simba imetangulia kuingia kambini, kama ilivyo kawaida yao imekimbilia Zanzibar ambako huweka kambi ya kujiandaa kuivaa Yanga na imeondoka Dar es Salaam ikiwa na msafara wa nyota wake 18.

Hans poppe aokoa jahazi

Awali safari hiyo ilikuwa katika hatihati kubwa kutokana na tatizo la ukosefu wa fedha, lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans poppe, alifanikisha kutoa fedha zilizookoa jahazi kwa kulipa mishahara ya wachezaji wote ya mwezi uliopita na safari ya kwenda Zanzibar ikafanyika.

Loga ndege, timu kwa boti

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’, alipanda ndege jana Jumatano asubuhi akitangulia Zanzibar huku akiwaachia timu wasaidizi wake, Selemani Matola na Idd Pazzi (Kocha wa Makipa) waliondoka na kikosi kwa boti, lakini imeelezwa timu nzima itarejea Dar kwa ndege kuhofia kuchoka.

Simba inataka heshima tu katika mchezo huo ambapo Loga ambaye ajira yake inaweza kuongezeka kupitia matokeo ya ushindi, ameliambia Mwanaspoti kwamba mechi hiyo ni ya kawaida kama zilivyo nyingine.

“Hakuna kipya katika mchezo huo, najua ni mechi inayozikutanisha timu zenye historia kubwa hapa nchini, tutaingia bila presha, tunataka kuwapa faraja mashabiki wetu hilo ndiyo kubwa,” alisema Loga.

Loga tayari ameshaonja ushindi mara moja katika mechi kama hiyo, ikumbukwe Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe mwishoni mwa mwaka jana, matokeo ambayo yaliotesha mbawa kibarua cha makocha wote wa Yanga waliokaa benchi katika mchezo huo wakiongozwa na Mholanzi Ernie Brandts.

Wekundu hao wameondoka na nyota wao wote muhimu wakiwamo makipa; Yaw Berko na Ivo Mapunda, mabeki ni Donald Mosoti, Joseph Owino, Issa Rashid, Nassoro Masoud ‘Chollo’ na William Lucian Gallas.

Viungo ni Jonas Mkude, Amri Kiemba, Henry Joseph, Awadh Juma, Ramadhan Singano ‘Messi’, Uhuru Seleman, Said Ndemla, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ huku washambuliaji wakiwa ni Amissi Tambwe na Zahoro Pazzi.

Maandalizi Yanga

Yanga kwa upande wake imeweka kambi yake katika hoteli ya Landmark, Kunduchi, jijini Dar es Salaam kuanzia jana Jumatano jioni mara tu baada ya kuwasili kutoka Arusha walikoifunga JKT Oljoro kwa mabao 2-1. Juzi Jumanne walicheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Pannone ya Moshi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 na jana Jumatano asubuhi walianza safari ya kurejea Dar es Salaam.

Timu hiyo inayofundishwa na Mholanzi, Hans Pluijm, ni wazi itakuwa na hasira za mara mbili; kwanza ni kupoteza taji lao la ubingwa lililotua Chamazi msimu huu, lakini la pili ambalo ni wazi litawaongeza hasira ni kupoteza mchezo wa mwisho uliomalizika kwa mabao 3-1 huku pia katika mechi ya kwanza ya ligi wakitoka sare ya mabao 3-3, matokeo yaliyoichanganya timu hiyo iliyokuwa ikiongoza kwa mabao 3 mpaka mapumziko.

Ukiacha makocha waliotimuliwa mpaka sasa, bado matokeo hayo yana wingu zito katika kikosi hicho hasa kwa upande wa wachezaji ambapo kipa wao aliyedaka mchezo huo, Ally Mustapha ‘Barthez’, aliingia katika tuhuma nzito kama ilivyo kwa kiungo Athuman Idd ‘Chuji’ na beki David Luhende ambao mpaka sasa bado wamekuwa wakikosa nafasi ya kucheza.

Okwi hayumo

Mpaka sasa, Yanga inaweza kukosa huduma ya nyota mmoja pekee ambaye ni mshambuliaji, Emmanuel Okwi, ambaye bado yupo katika mgomo akidai kukamilishiwa fedha zake za usajili.

Imeelezwa kuwa nyota huyo amegoma kupokea Dola 20,000 (Sh32 milioni) zikiwa ni sehemu ya Dola 50,000 anazodai, akisisitiza mpaka alipwe chake chote.

Tayari kocha Pluijm ameshasema kuwa kuna ugumu kwa mchezaji huyo kuingizwa kambini ili acheze mechi hiyo kutokana na kukosa mazoezi ya zaidi ya wiki moja na nusu. Lakini pia kiungo Haruna Niyonzima licha ya kwamba afya yake imeimarika bado hajaitwa kambini.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Pluijm, ambaye bado hajajua joto la mechi kama hiyo, alisema anataka kuhakikisha anashinda lakini akageuka mkali baada ya kusikia kuwa Loga ametamka kuwa kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinauchukulia mchezo huo kwa wepesi.

Kikosi cha Yanga kilichoingi a kambini jana ni pamoja na makipa Deogratias Munishi ‘Dida’, Ally Mustapha ‘Barthez’, mabeki ni Mbuyu Twite,Oscar Joshua,Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, viungo ni Frank Domayo,Simon Msuva, Hassan Dilunga,Hamis Thabit, Nizar Khalfan, Salum Telela.

Washambuliaji ni Mrisho Ngasa,Didier Kavumbagu, Jerry Tegete,Hussein Javu naHamis Kiiza lakini kipa Juma Kaseja hayumo katika kambi hiyo pamoja na beki David Luhende.

Rekodi za Loga, Pluijm

Makocha hawa watakutana kwa mara ya kwanza katika mchezo huo hapa nchini, wote wana ajira za miezi sita zinazoelekea ukingoni, atakayeshinda atakuwa na nafasi ya mkataba mpya.

Loga alipoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Pluijm walipokuwa Ghana ambako Loga alikuwa akiifundisha Hearts Of Oak huku Pluijm akiwa na Berekum Chelsea ambapo Pluijm alishinda mabao 4-2.