Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamia waipokea Simba uwanja wa ndege mvua ikinyesha

Muktasari:

  • Kikosi cha Simba kimerudi nchini kikiwa na furaha  kubwa baada ya kufuzu kwa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo, kufuatia ushindi wa  bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch.

MAMIA ya mashabiki wa Simba  wamejitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), usiku huu kuwapokea wachezaji waliorejea kutoka Afrika Kusini baada ya kuandika historia mpya kwenye soka la Afrika.

Kikosi cha Simba kimerudi nchini kikiwa na furaha  kubwa baada ya kufuzu kwa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo, kufuatia ushindi wa  bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch.

Licha ya mvua kunyesha, mashabiki hawakujali waliendelea kuimba kwa shangwe, kupiga vuvuzela na kucheza ngoma zilizopigwa na vikundi maalumu vilivyoandaliwa kwa ajili ya mapokezi hayo, wakionyesha mapenzi ya dhati kwa timu yao.

Wakiwa wamevalia jezi za Simba, mashabiki walijaza katika mlango wa kutokea abiria, wakisubiri kwa hamu kuwalaki wachezaji waliopigania heshima ya klabu yao kimataifa.

Mara baada ya kurejea nchini, Simba sasa itaanza maandalizi kwa ajili ya fainali ambapo itachuana na RS Berkane. Mechi ya kwanza itachezwa Mei 17 huko Morocco, kabla ya mchezo wa marudiano Mei 25 hapa nchini.

Safari ya Simba kuelekea kutwaa taji la Shirikisho Afrika inaonekana kuwa ya kihistoria, huku matumaini ya Watanzania yakiwa juu wakisubiri kwa hamu kuona timu yao ikitimiza ndoto ya kuwa mabingwa