Manara rasmi Yanga

ALIYEKUWA ofisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amejiunga na klabu ya Yanga leo Jumanne Agosti 24, 2021 katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Manara awali aliondolewa katika wadhifa wa kuwa ofisa habari wa klabu ya Simba baada ya kutokea sintofahamu baina yake na uongozi wa klabu hiyo.
Manara alifika ukumbini hapa akiongozana na kaimu Katibu mkuu wa Yanga, Haji Manara na kukaribishwa na mhamasishaji Antonio Nugaz.
Manara aliingia ukumbini hapo akiambatana na familia yake huku sura yake ikiwa na furaha muda wote.