Manara: Sikuwa na namna

ALIYEKUWA afisa habari wa Simba, Haji Manara amesema hakuwa na namna ya kufanya maamuzi ya kujiunga na Yanga ambayo ni klabu kubwa Afrika Mashariki na Kati.
SOMA: Manara rasmi Yanga
Manara amesema yeye ni mtu anayefanya kazi kwa weledi hivyo anaamini kabisa kazi yake ataifanya kwa utulivu.
“Nilikuwa na ofa nyingi lakini walipokuja viongozi wa Yanga nilijiuliza maswali mengi lakini nilipouliza kuhusu malengo yao waliniambia wanataka mataji na mimi napenda mataji,” anasema Manara.
Manara amesema yeye ni kama mchezaji hivyo kuwepo kwake Yanga anaamini ataifanya kazi yake kwa weledi mkubwa.
“Niliteseka sana huko nilipokuwa na sitaki kabisa kuongelea kwa sababu nilishasema kabisa waliyonifanyia,” anasema Manara.