Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayanga atenga siku nane Mashujaa

Muktasari:

  • Timu hiyo iliyopo nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 30 baada ya mechi 26, itaanza dakika 90 za kwanza dhidi ya Simba ambayo ina michezo minane mkononi kutokana na kuwa kwenye majukumu ya michuano ya kimataifa.

MASHUJAA imebakiwa na dakika 360 za kibabe kumaliza msimu wa 2024/25, huku kocha wa timu hiyo, Salum Mayanga akisisitiza anataka kutumia siku nane  kujipanga ili kuona wanatoboaje mbele ya Simba.

Timu hiyo iliyopo nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 30 baada ya mechi 26, itaanza dakika 90 za kwanza dhidi ya Simba ambayo ina michezo minane mkononi kutokana na kuwa kwenye majukumu ya michuano ya kimataifa.

Hesabu za Mayanga kushinda mechi zote zilifeli katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo baada ya kuambulia kichapo cha mabao 2-1 ugenini, sasa imejichimbia kujiweka tayari kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Simba utakaochezwa Mei 2, 2025 kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mayanga alisema timu yake ina kibarua kigumu ambacho wanatakiwa kuhakikisha ndani ya siku nane tu mambo yanakaa sawa.

“Tunaanza na timu bora ambayo ina matokeo mazuri kwenye michuano inayoshiriki, ili kukabiliana nayo tunahitaji maandalizi bora, hicho ndicho ninakifanya sasa na ukizingatia tukiwa nyumbani tulikubali kupoteza kwa bao 1-0.

“Ni mechi kubwa na ya ushindani kwani tutacheza na timu ambayo inarejea kusaka nafasi ya kutwaa taji ambalo wamelipoteza kwa misimu mitatu na sisi tunapambana kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi msimu ujao, hivyo hautakuwa mchezo rahisi,” alisema.

Alisema mbali na mchezo huo ambao kwao wanauchukulia kama fainali, wana mechi nyingine tatu ngumu dhidi ya Kagera Sugar, KMC na JKT Tanzania ambao pia wanaitaka nafasi ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

“Huu ni mzunguko wa lala salama, hakuna mechi nyepesi, zote ni ngumu.” alisema.