Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mazoezi ya Moyes kero kwa Van Persie

Straika Mdachi, Robin van Persie

Muktasari:

Yeye ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita kwenye Ligi Kuu, lakini msimu huu anazidiwa hata na viungo kama Aaron Ramsey kwa ufungaji, huku akienda sambamba na viungo wengine kama Oscar na Yaya Toure, ambao nao wana mabao manne kila mmoja.

STRAIKA Mdachi, Robin van Persie ana mabao manne tu kwenye Ligi Kuu hadi sasa baada ya mechi nane. Amezidiwa na mastraika wengine kama Daniel Sturridge, Sergio Aguero na Loic Remy.

Yeye ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita kwenye Ligi Kuu, lakini msimu huu anazidiwa hata na viungo kama Aaron Ramsey kwa ufungaji, huku akienda sambamba na viungo wengine kama Oscar na Yaya Toure, ambao nao wana mabao manne kila mmoja.

Hata hivyo, wakati Van Persie akionekana kushuka kwenye kiwango chake cha kupiga mabao kama ilivyokuwa msimu uliopita, ambapo alikuwa msaada mkubwa kwa Manchester United hata ilipokuwa kwenye hali ngumu ndani ya uwanja, Mdachi huyo ana malalamiko makubwa.

Mabao yamekuwa tatizo kwenye kikosi cha Manchester United, hadi sasa wamefunga mabao 11 tu, huku wakiruhusu 10 kwenye nyavu zao, wakati wapinzani wao kama Arsenal wana mabao 18 ya kufunga na tisa ya kufungwa na Manchester City imefunga 20 na kufungwa tisa tu.

Hadi sasa, Manchester United imezidiwa na timu zote vigogo kwa mabao ya kushinda. Liverpool imefunga mabao 13, Chelsea 14, huku timu za Everton na Swansea City zikiifunika pia timu hiyo ya David Moyes kwa mabao msimu huu.

Kwa nini Van Persie hafungi?

Tangu msimu huu kuanza, Van Persie analalamika kwamba kuna kitu hakipo sawa kwenye mazoezi ya Moyes kuwa ni magumu sana na kumsababishia majeruhi ya mara kwa mara.

Wakati straika huyo anatoka Arsenal na kutua Manchester United mwaka jana, wengi waliamini kocha Alex Ferguson aliingia mkenge kumsajili kwa pesa nyingi huku ikifahamika wazi kwamba mchezaji huyo ana tatizo la majeruhi. Lakini, Ferguson alimwaandalia programu maalumu ya mazoezi iliyomfanya acheze msimu mzima bila ya kupata majeruhi na alifunga mabao mengi kila alipotinga uwanjani.

Moyes anamharibu Van Persie kwa kumfanyisha mazoezi magumu yanayomtonesha majeraha na kumfanya apoteze makali yake ya kutikisa nyavu, kwa sababu hachezi akiwa yupo fiti kwa asilimia mia.

Straika mwingine wa kikosi hicho, Wayne Rooney naye amekiri kuwa mazoezi ya Moyes ni magumu kiasi cha kuwafanya wachezaji kuchoka wanapokuwa uwanjani.

Amkumbuka Meulensteen

Mbinu za ufundishaji wa Moyes ndicho kitu kinachomkera Van Persie. Staa huyo aliwaambia marafiki zake kwamba benchi la ufundi la timu hiyo kwa sasa linawafanyisha wachezaji mazoezi mengi ya kukimbia tofauti na ilivyokuwa chini ya Ferguson.

Fowadi huyo aliyeibuka kinara wa mabao Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululizo, aliwaambia marafiki zake anashangaa kwa nini kocha aliyekuwa msaidizi wa Ferguson, Rene Meulensteen, aliyekuwa akikinoa kikosi cha kwanza, ambaye ni Mdachi mwenzake hakubaki kwenye timu hiyo na kuwa chini ya Moyes kwa sababu alikuwa anafahamu namna ya kumfanya kuwa fiti muda wote.

Azozana na Moyes

Imeripotiwa kwamba Van Persie na Moyes walianzisha mzozo mkubwa wakati wa kujifua kwa ajili ya mechi ya wapinzani wao Manchester City (Manchester derby) kwa bsababu aina ya mazoezi yake yalimsababishia majeruhi na hivyo kukosa mchezo huo uliomalizika kwa Manchester United kulambwa mabao 4-1.

Kukosa mechi hiyo pia kulitibua rekodi yake ya kucheza mechi 90 mfululizo za Ligi Kuu tangu alipokuwa Arsenal, ambapo mara ya mwisho kukosa mechi ya ligi ilikuwa Machi 2011.

Van Persie alilalamikia ufundishaji wa Moyes kwamba mazoezi yake amemsababishia kuwa majeruhi, huku kocha huyo Mskochi akidai kwamba hawakuwa kwenye hali nzuri na mchezaji huyo baada ya tukio hilo kuonekana kuwa kubwa.

Van Persie alikosa pia mechi ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool na alianzia benchi kwenye mechi ya kichapo cha mabao 2-1 kwenye Ligi Kuu dhidi ya West Brom. Van Persie alisema mazoezi wanayofanya katika kujiandaa na mechi yamekuwa magumu kiasi ambacho hayawajengi zaidi kuwaharibia mfumo wa kiuchezaji na kuwachosha miili.

“Ni mambo tofauti sana tangu David Moyes na wasaidizi wake walipokuja,” anasema Wayne Rooney na kuongeza: “Mazoezi yamekuwa tofauti, staili ni tofauti hata akili ya kiuchezaji nayo anataka tuwe tofauti. Kwa kusema ukweli, mazoezi yamekuwa magumu sana. Tunakimbia sana. Tunakimbia mbio ndefu, fupi na zile za kasi sana. Sawa zinaniweka fiti, lakini kubwa ni kwamba nafurahia soka ninalocheza.”