Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya City yampigia hesabu beki Mzenji

MBEYA Pict

Muktasari:

  • Mbeya City itakayoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ya Ligi ya Championship na kupanda daraja, inawania saini ya nyota huyo sambamba na Dodoma Jiji, Pamba Jiji na Namungo FC.

KATIKA mikakati ya kuimarisha kikosi, imeelezwa kwamba Mbeya City ni kati ya timu nne zinazowania saini ya beki wa kati wa Singida Black Stars, Mzanzibar Mukrim Issa ‘Miranda’.

Mbeya City itakayoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ya Ligi ya Championship na kupanda daraja, inawania saini ya nyota huyo sambamba na Dodoma Jiji, Pamba Jiji na Namungo FC.

Nyota huyo ambaye kwa sasa anaichezea Dodoma Jiji kwa mkopo akitokea Singida Black Stars, amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na kikosi hicho, japo taarifa zinaeleza kuna uwezekano akafunguliwa mlango wa kutokea ili akapate changamoto mpya.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata kutoka kwa watu wa karibu na mchezaji huyo aliyeichezea pia Coastal Union kabla ya kutua Dodoma Jiji, zinaeleza Dodoma Jiji imenogewa na huduma Miranda hivyo inamuhitaji moja kwa moja, japo kuna ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao ikiwamo Mbeya City.

“Tunaamini tuna nafasi ya kumpata kwa sababu Singida sio rahisi kurudi kutokana na ushindani uliopo pale, hivyo kwa sasa tunasubiri msimu huu wa Ligi Kuu Bara ufikie mwisho ndio tuanze huo mchakato vizuri,” alisema kiongozi mmoja wa Dodoma Jiji.

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Ally Nnunduma, alisema kinachoendelea kwa sasa ni kuifanyia kazi ripoti ya benchi la ufundi kwa haraka iwezekanavyo, hivyo mashabiki wa kikosi hicho wawe na subra katika kipindi hiki.

Tangu ajiunge katika dirisha dogo la usajili msimu huu, amempindua Mkongomani Heritier Lulihoshi aliyekuwa anaanzishwa.