Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda mzuka mwingi DR Congo

Mgunda Pict

Muktasari:

  • Japo Mgunda hakutaja moja kwa moja anakwenda kujiunga na AS Vita ya DR Congo kama ulivyoeleza uongozi wa Mashujaa kupitia Ofisa Habari Hamis Mwalyango kumalizana na klabu hiyo na mchezaji, lakini mshambuliaji huyo anatua timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya DR Congo.

MSHAMBULIAJI Ismail Mgunda amesema kitendo cha Mashujaa kukubali kumuachia kwenda kutafuta changamoto mpya kinamsaidia kuendelea kumjenga na kukuza kiwango na kipaji chake.

Japo Mgunda hakutaja moja kwa moja anakwenda kujiunga na AS Vita ya DR Congo kama ulivyoeleza uongozi wa Mashujaa kupitia Ofisa Habari Hamis Mwalyango kumalizana na klabu hiyo na mchezaji, lakini mshambuliaji huyo anatua timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya DR Congo.

“Tumemalizana na AS Vita pamoja na mchezaji ndio maana tumetangaza hatakuwa sehemu ya kikosi chetu. Tumemtakia kila la heri mapambano yake mapya,” alisema Mwalyango.

Hata hivyo, Mgunda alisema bado hajasaini ofa ya AS Vita na kuna timu nyingine inayohitaji huduma yake na wikiendi hii anaweza akaondoka nchini akikataa kutaja anakwenda wapi.

“Ielewele bado sijasaini AS Vita ofa ipo mezani, ingawa kila kitu kikienda sawa nitasaini,” alisema.

“Fursa niliyopata ya kwenda nje inanipa nguvu na kuongeza bidii. Natamani uwe mwanzo wa kufika mbali zaidi ya hatua hii.”