Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Minziro: Tuna dakika 360 ngumu

MINZIRO Pict

Muktasari:

  • Pamba imerejea Ligi Kuu msimu huu ikiwa ni zaidi ya miaka 23 tangu iliposhuka daraja mwaka 2001 na kwa sasa ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 27 kupitia mechi 26, pointi inazoifanya isiwe mahali salama kwani kama wasipopambana wataangukia katika play-off ya kuepuka kushuka daraja.

KOCHA Mkuu wa Pamba Jiji, Fred Minziro amesema hatma ya timu hiyo ipo mikononi mwa mechi nne ambazo ni sawa na dakika 360 za kufungia msimu ili kujihakikishia kubaki Ligi Kuu Bara msimu ujao na ameshazungumza na wachezaji kuweza kupanga mikakati ya kibabe.

Pamba imerejea Ligi Kuu msimu huu ikiwa ni zaidi ya miaka 23 tangu iliposhuka daraja mwaka 2001 na kwa sasa ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 27 kupitia mechi 26, pointi inazoifanya isiwe mahali salama kwani kama wasipopambana wataangukia katika play-off ya kuepuka kushuka daraja.

Timu mbili zinazoshika nafasi ya 13 na 14 ndizo zinazocheza play-off kili kubaki Ligi Kuu na ile inayopoteza baada ya kukutana wenyewe kwa wenyewe, itacheza mechi na mshindi wa mechi ya Ligi ya Championship na ikipoteza inashuka daraja na kuipisha mpinzani na ikishinda itasalia kwa msimu ujao.

Tayari KenGold iliyopo mkiani mwa msimamo imeshashuka rasmi na imesalia nafasi moja ya kuungana nao kucheza Championship kwa msimu ujao, kitu kinachomtisha Minziro mwenye rekodi tamu ya kupandisha timu kadhaa katika Ligi Kuu akiwa sambamba na Mbwana Makatta na makocha wengine.

Akizungumza na Mwanaspoti, Minziro alisema Pamba haipo katika nafasi nzuri wanachokifanya sasa ni kuandaa timu ya ushindi kwa kila  mechi ili kujihakikishia nafasi ya kucheza msimu ujao huku akiweka wazi kuwa hakuna kinachoshindikana wakiweka mikakati imara.

“Ukiitaja Simba pekee unazikosea heshima timu nyingine tatu ambazo tunatarajia kukutana nazo sina mchezo rahisi ni kweli KenGold imeshuka haijabaki kugawa pointi kwenye mechi zilizobaki watacheza kushuka kwa heshima natarajia mechi ngumu na ndio zilizoshika hatma yangu,” alisema Minziro na kuongeza;

“Tumeshaanza mikakati na kusuka njia sahihi ambazo tutapita ili tupate matokeo kwenye mechi hizo zilizobaki naushukuru uongozi kwa kunishika mkono kutokana na bonasi zinazotolewa kuhusu wapinzani wote ni bora na wana mbinu nzuri tunafanyia kazi mazoezini ili tuweze kuvuka mitego yao.”

DK 360 ZA MOTO

Pamba kwa sasa ipo katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba uliopangwa kupigwa Mei 8, mwaka huu itakuwa ugenini dhidi ya Simba kabla ya kuvaana na KenGold iliyokata tiketi ya kushuka daraja, mechi itakayopigwa Mei 13 kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mei 21 Pamba itakuwa na kibarua dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kisha kumalizana na KMC kwenye uwanja huo Mei 25, huku kila moja ikiwa katika hali mbaya kwa sasa.