Mlandizi Queens kama KenGold tu

Muktasari:
- Timu hiyo imeshuka rasmi na inarejea Ligi daraja la kwanza ilipotoka msimu uliopita kutokana na mwenendo mbaya wa Ligi Kuu tangu msimu uanze.
HATIMAYE Mlandizi Queens imeshuka daraja rasmi baada ya kucheza mechi 15 bila ushindi ikitoka sare moja sawa na Ken Gold iliyoshuka Ligi Kuu baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union wikiendi iliyopita.
Timu hiyo imeshuka rasmi na inarejea Ligi daraja la kwanza ilipotoka msimu uliopita kutokana na mwenendo mbaya wa Ligi Kuu tangu msimu uanze.
Mlandizi ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake 2017/18 kisha baadae JKT Queens ikaipokonya na kutwaa mara mbili mfululizo.
Kwa sasa inakamilisha ratiba ya mechi tatu zilizosalia ikianza na Alliance Girls, Mashujaa Queens na Fountain Gate.
Mbali na kuweka rekodi mbaya Ligi Kuu ya kukusanya pointi moja pekee lakini ndio timu iliyoruhusu mabao mengi 70.
Kiufupi Mlandizi ina wastani wa kuruhusu mabao manne kwa kila mchezo na imefunga mabao sita.