Mrithi wa Chama Simba huyu hapa

SIMBA inaendelea kushusha vifaa vipya, kusuka kikosi chao cha msimu ujao na leo Jumamosi ya Agosti 14, 2021 imeshamtambulisha kiungo kutoka Senegal, Pape Ousmane Sekho.
Sekho amesajiliwa kuziba nafasi ya kiungo fundi Clatous Chama, ambaye ameuzwa katika klabu ya Rsb Berkane ya nchini Morocco.
Huyu ni mchezaji wa tatu wa kigeni, kutambulishwa na Wekundu wa Msimbazi, alianza Peter Banda ambaye tayari kakabidhiwa jezi namba 11 ya Luis Miquissone aliyeuzwa Al Ahly ya Misri, kisha alifuatia Duncan Nyoni kutoka Malawi, anacheza nafasi ya winga mshambuliaji.
Simba imekwenda kupiga kambi nchini Morocco, kujifua kwa ajili ya msimu ujao, ikiwa na rekodi ya kuchukua mataji ya Ligi Kuu Bara, mara nne mfululizo na kutoa wafungaji bora.
Msimu wa 2017/18 alichukua Emmanuel Okwi na mabao 20, 2018/19 Meddie Kagere alimaliza na mabao 23, akatetea tena 2019/2020 alimaliza na mabao 22 na msimu ulioisha ni John Bocco alimaliza na mabao 16.