Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa noma, yarejea Ligi Kuu baada ya siku 332

Muktasari:

  • Timu mbili zinazoongoza msimamo wa Ligi ya Championship mwishoni mwa msimu, zinapanda Ligi Kuu moja kwa moja.

Sare ya bao 1-1, iliyoipata Mtibwa Sugar ugenini dhidi ya Bigman FC kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi, imeifanya timu hiyo kurejea rasmi Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, huku ikiwa ya kwanza kukata tiketi hiyo, ikisaliwa na michezo miwili mkononi kuhitimisha msimu wa 2024-2025.

Mtibwa iliyoshuka daraja msimu uliopita sambamba na Geita Gold, imepanda kufuatia Stand United kulazimishwa suluhu ugenini na Cosmopolitan.

Iko hivi, Mtibwa Sugar kwa sasa imefikisha pointi 67 baada ya kucheza michezo 28, hivyo timu pekee inayoweza kuzifikia ni Mbeya City iliyoichapa Geita Gold mabao 3-2, ambapo ikishinda mechi zake zote mbili zilizobakia itafikisha pointi 68.

Kwa maana hiyo, suluhu ya Stand United inaiweka nafasi ya tatu na pointi 59 ambapo hata ikishinda michezo yake miwili iliyobakia itaishia na 65, hivyo itakuwa na kinyang'anyiro cha kuwania michezo ya 'Play-Off' kusaka tiketi ya kupanda tu.

Katika michezo mingine iliyopigwa leo ya raundi ya 28, maafande wa Transit Camp wakiwa kwenye Uwanja wa Kituo cha TFF Kigamboni jijini Dar es Salaam, imeibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1, dhidi ya kikosi cha TMA FC kutoka jijini Arusha.

Green Warriors ikiwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam, imekubali kichapo cha bao 1-0, dhidi ya

Biashara United, huku Songea United ikiwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Ruvuma imeichapa Polisi Tanzania kwa mabao 2-0.

Kiluvya United ikiwa kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani imeibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Mbuni FC ya Arusha, huku Mbeya Kwanza ikicheza nyumbani Nangwanda Sijaona mjini Mtwara imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na African Sports.