Mwongozo wa ubashiri mtandaoni: Michezo ipi ya kubashiri

Imepita kipindi kirefu cha mpito kutokana na majanga ya mlipuko wa Covid19 lakini kwa sasa michezo yote mikubwa duniani imerudi kwenye mstari wake kama ilivyokuwa hapo awali.
Changamotombalimbali ikiwemo mashindano kutofanyika au kughairishwa kwa mechi kwa sasa zinaonekana kuisha kabisa na bashiri za mtandaoni zipo tayari kwa ajili ya kufanya ambacho huwa zinafanya kila siku.
Kama bado unahisi kuna changamoto na haujui ni kipi cha kufanya ni vyema ukapitia na kujua ni michezo gani ambayo utaitumia kwa ajili ya kubashiri. Kuna fursa mbalimbali ambazo zinavutia macho ya watu wengi na kwa maana hiyo ni mwiko kurudi nyuma bila sababu ya msingi.
Ukiachilia mbali na kuwa na umaarufu lakini pia ni hakika baadhi ya michezo inaweza kubashirika kwa urahisi zaidi Fursa ya Kubashiri Mtandaoni kutokana na aina ya masoko, odi na kadhalika.
Kama unahisi kuna mchezo fulani wa kubashiri unaendana kabisa na wewe na unataka uanze kubashiri kwa mara ya kwanza basi unashauriwa kufanya yafuatayo ili uanze kwa ufasaha.
Jinsi ya kubashiri kwa mafanikio
Kila mbashiri kwa sasa anavutiwa sana na fursa mpya, masoko na michezo mingi. Idadi ya watu wapya wanaoingia kwenye kubashiri kila msimu inaongezeka maradufu.
Kama unafikiria kuingia katika jamii hiyo kwanza kabisa inabidi utafute mchezo ambao unaumudu kwa kiasi kikubwa. Ni rahisi zaidi kubashiri kwenye michezo unayoijua kwa kiasi kikubwa kwani hii itakusaidia kuyatambua masoko ya michezo husika.
Soka
Mpira wa miguu ndio mchezo ambao unakusanya watu wengi kwa idadi katika kila nyanja. Kwenye upande wa kubashiri mpira wa miguu ndio mchezo ambao upo juu ukiwa na wafuasi wengi ukilinganisha na michezo mingine iliyopo katika orodha.
Kwa kawaida kubashiri kandanda ndio njia rahisi kwa wanaonza michezo ya kubashiri hata kwa wale ambao ni wazoefu. Ni mchezo ambao una masoko ambayo yanaeleweka kwa wote.
Kitu kimoja ambacho kinarahisisha kwenye mpira wa miguu hasa kwa wanaoanza kubashiri ni upatikanaji mwepesi wa vitendea kazi na matukio ya mara kwa mara.
Pia ni uwepo wa taarifa kuhusu timu na wachezaji mbalimbali wa kandanda ambazo zinawafikia watu wengi na kufanya kazi ya kubashiri kuwa rahisi.
Kitu kingine kinachovutia katika soka hasa kwa watu wapya kwenye masuala ya ubashiri ni kwasababu mchezo wa mpira wa miguu unahusishwa na soko kubwa na odi za kuvutia zaidi. Pia mchezo huu umekuwa ni wa moja kwa moja na hivyo haihitajiki uelewa au akili kubwa sana ili uweze kufanya bashiri zako.
Baadhi tu ya bashiri zako zinaweza kukupa nafasi kubwa ya kushinda. Lakini pia uweke akilini kwamba kuna muda mchezo huu wa mpira wa miguu unajumuishwa na odi ndogo na hivyo malipo yake yanakuwa sio makubwa. Lakini ni vyema ukaanza taratatibu kabla ya kuja kuwa na uwezo mkubwa katika bashiri zako.
Muongozo kwa aanzaye kubashiri kwenye soka
- Over/under- Unatakiwa ubashiri kwa kusema kuwa idadi ya mabao itakuwa kubwa au ndogo “Over-Under” katika mechi husika. Kama unahisi kutakuwa na mabao mengi basi unaweka Over na kama unahisi yatakuwa machache unaweka Under.
- Mchezaji wa kwanza kufunga- katika majina ambayo utawekewa unatakiwa kubashiri ni mchezaji gani atakuwa wa kwanza kufunga na kama unaweza kuongeza ufundi basi utabashiri na muda sahihi ambao atafunga bao hilo la kwanza.
- Double Chance Betting — hii ni miongoni mwa bashiri nyepesi kwa watuamiaji wapya ambapo unaweza ukabshiri aina mbili ya matokea katika mechi moja. Unaweza ukachagua matokeo mawili kati ya matatu ambayo huwa yanatokea kwenye mpira wa miguu. Mfano unaweza ukachagua kuwa timu ya nyumbani itashinda au itakwenda sare katika mchezo husika 1/X au unaweza ukachagua kwamba timu ya nyumbani itashinda lakini wakati huo huo ukasema kuwa timu ya ugenini itashinda ½.
- BTTS Bets — Hili ni soko ambalo linamtaka mbashiri aseme kama timu zote zitamaliza mechi husika zikiwa zimefungana magoli bila ya kujali timu gani itapata ushindi au kufungwa. Ikitokea hivyo basi itakuwa umeshinda bashiri yako.
Tenesi
Inapotokea kuna mchezaji bora wa miaka mingi hii huwa inarahisisha kuweka bashiri hasa kwa watu wanaonza kubashiri kwa michezo ya tenesi.
Jina la mtu kama Novak Djokovic, Roger Federer na Rafael Nadal haya ni miongoni mwa majina makubwa katika mchezo wa tenesi.
Hata hivyo, hii haina maana kwamba wachezaji hawa hawewezi kufungwa. Lakini hii ya kuangalia wachezaji wakubwa ni miongoni mwa njia nyepesi zinazofanya mchezo wa tenesi uonekane ni rahisi kuubashiri.
Katika vitu vyote muhimu lakini pia ni vizuri kuangalia uwezo wa wachezaji husika na jinsi walivyocheza katika mechi mbalimbali na hii inakurahisishia sana katika kazi ya kubashiri mtandaoni.
Uwezo mkubwa mbao mara kwa mara umekuwa ukioneshwa na wale magwiji wa mchezo wa tenesi katika michuano mbalimbali ndio umefanya mchezo huu kuonekana ni miongoni mwa michezo rahisi kubashiri kwasababu ni mara chache kukuta wanapoteza michezo yao.
Tenesi pia ni miongoni mwa michezo ambayo inatoa masoko mengi ya kubashiri ambayo yanaweza kukuvutia na ukaanza.
Muongozo kwa ambaye anaanza kubashiri kwenye tenesi
- Match Betting — Hili ni soko rahisi zaidi kati ya yote ambalo lina mtaka mbashiri kuweza kusema ni mchezaji gani atashinda mchezo katika mchi husika.
- Outright Betting — Hii ni soko ambalo halina tofauti sana na hilo hapo juu. Tofauti yake ni kwamba wakati mchezaji unayemchagua ashinde mechi lakini pia unaweza kumchagua awe bingwa wa michuano husika. Katika hili unaangalia tu mchezaji gani ambaye amepewa odi ndogo maana yake huyo anapewa nafasi kubwa ya kushinda wakati wale ambao hawapewi nafasi kubwa ya kushinda ubingwa utaona odi zao ni kubwa.
- Over/Under — katika mchezo wa tenesi kuna kitu kinaitwa seti ambazo kikawaida huwa ni tatu. Lakini kwenye seti hizi tatu anatakiwa apatikane mshindi aliyekusanya idadi ya jumla ya ushindi isiyopungua sita kama idadi hiyo haijafikiwa basi seti zitaongezeka hadi bingwa apatikane. Kwa hiyo unavyobashiri Over/Under kwenye mchezo wa tenesi unakuwa unabashiri kama kutakuwa na seti nyingi au chache kulingana na masoko uliyowekewa. Ukiweka Over maana yake mchezo utakuwa na seti nyingi na ukiwaweka Under maana yake kutakuwa na seti chache.
Mbio za farasi
Katika mchezo wa mbio za farasi wabishiri wa muda mrefu imekuwa ni ngumu sana kwa kubashiri kuliko wale wabishiri wapya. Hii inatokana na kwamba wabashiri wa muda mrefu wamekuwa na tabia ya kukariri na wakati matokeo katika mchezo huu yamekuwa hayatabiriki kwa wepesi.
Kabla ya kuweka bashiri yako ya kwanza katika mchezo huu unatakiwa kuzingatia baadhi ya vitu vya msingi. Kwanza unatakiwa kuangalia mbio mbalimbali ambazo zipo miongoni mwa zile maaruf zaidi.
- Kentucky Derby
- Preakness Stakes
- Belmont Stakes
- Breeders’ Cup
Ukishaamua tayari ni mbio zipi ambazo ni nzuri zaidi kwako, hatua ifuatayo angalia masoko ambayo yanakufaa na kuna baadhi ya miongozo ambayo unaweza ukaanza nayo kama ifuatavyo.
Muongozo kwa anayeanza kubashiri kwenye mbio za farasi
- Place Betting — Soko hili ni kwamba unambashiria farasi ambaye atamaliza nafasi ya kwanza au ya pili ili uweze kushinda.
- Show Betting — Soko hili ni rahisi kati ya yote kwani utahitajika kubashiri farasi mmoja atakayeweza kumaliza katika nafasi tatu za juu na hapo utakuwa umeshinda bashiri yako.
- Win Betting — Soko hili utahitajika kumchagua farasi ambaye atakuwa wa kwanza kuanzia mwanzo wa mbio hadi mwisho. Na hii ni miongoni mwa bashiri ngumu katika mchezo huu.
Michezo mingine mingi inaweza kuwa kivutio kikubwa katika kubashiri lakini kubwa zaidi katika kila mchezo unaotaka kubashiri hakikisha unaangalia vizuri masoko, odi na matukio yenyewe ya kimichezo.
Katika kila mchezo unaotarajia kuingia kubashiri hakikisha unakuwa una maamuzi yaliyokamilika na bashiri zako.
Majaribio yanamfanya mtu kuwa bora zaidi badala ya kukaa pembeni na kusubiri matokeo. Ingia sasa katika mchakato huku ukiwa unajifunza wakati unafurahia.
Jinsi ya kubashiri kwenye michezo ya NBA
- Place Bet- Soko kuu na la kwanza kabisa katika mchezo huu ni kuweza kubashiri timu ipi ambayo itaibuka na ushindi katika mechi husika. Na jinsi ya kuibuka na ushindi maana yake ni kushinda vikapu vingi zaidi kuliko mpinzani wako. Mara zote timu ambayo inapewa nafasi kubwa ya kushinda huwa inapewa odi chache kulinganisha na timu ambayo inaonekana ni dhafifu katika mchezo.
- Over/Under- Kama ilivyo katika michezo mingine kwenye mpira wa kikapu pia kuna soko la Over/Under ambapo unatakiwa kubashiri wingi au uchache wa vikapu kwa timu moja au kwa ujumla katika mchezo mzima. Over maana yake idadi ya vikapu itazidi idadi ambayo imewekwa katika soko na Under maana yake idadi ya vikapu inatakiwa kuwa chini.
- Mchezaji- Pia unaweza kumtaja mchezaji ambaye atafunga vikapu vingi zaidi katika mchezo na hii wachezaji nyota kama Stephen Curry huwa wanakuwa na odi ndogo ukilinganisha na wengine