Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzenji ajipa matumaini Transit Camp

MZENJI Pict

Muktasari:

  • Ahmada alisema wapinzani wao wanawapa presha kutokana na kutopishana pia pointi nyingi, ingawa kumekuwa na mwenendo mzuri wa kikosi hicho tangu awasili, jambo linalompa matumaini ya kukinusuru.

KOCHA wa Transit Camp, Mzanzibar Ramadhan Ahmada Idd amesema ushindi wa kikosi hicho wa mabao 4-1, dhidi ya TMA FC ya Arusha umewapa matumaini makubwa ya kuipigania timu hiyo, ili kuondokana na janga la kucheza ‘Play-Off’.

Ahmada alisema wapinzani wao wanawapa presha kutokana na kutopishana pia pointi nyingi, ingawa kumekuwa na mwenendo mzuri wa kikosi hicho tangu awasili, jambo linalompa matumaini ya kukinusuru.

“Hali yetu ni nzuri lakini tuna kazi kubwa ya kufanya ili kuepuka kucheza michezo ya mtoano kwa sababu presha huongezeka zaidi kutokana na mahitaji ya kila timu, muhimu ni kushinda mechi zilizobakia kisha tuangalie tutakapoishia,” alisema.

Ahmada aliyewahi kuifundisha Kipanga FC na Sharp Boys zote za visiwani Zanzibar, ni kocha wa tatu kukifundisha kikosi hicho msimu huu, baada ya awali kuanza na Ally Ally, kisha baadae akateuliwa Stephen Matata aliyeondoka mwenyewe pia.

Kikosi hicho kiko nafasi ya 13 ambayo ni ya Play-Off kusaka kubakia Ligi ya Championship msimu ujao na pointi 20 sawa na Cosmopolitan ya 14, baada ya kushinda michezo mitano, sare mitano na kupoteza 18 kati ya 28.