Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndondo kuwaponza nyota Yanga

Mbuyu Twite.PICHA|MAKTABA

Muktasari:

Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alipoulizwa kuhusu hilo alisema kuwa watafanya uchunguzi na wakibainika kukutwa na kosa basi hatua dhidi yao zitachukuliwa.

NYOTA wa Yanga wakiwemo Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete na David Luhende huenda wakaadhibiwa kwa kosa la kucheza mechi ya mchangani maarufu kama ndondo.Wachezaji hao walionekana juzi Jumanne wakiichezea timu ya Liverpool iliyokuwa inamenyana na Galatasaray katika fainali za Ligi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtakala uliopo Makangarawe, Temeke ambayo mshindi anakabidhiwa jezi.

Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Makaburi ya Jiji, Makangarawe, ambapo Liverpool iliongoza kwa mabao 2-1 kabla ya mwamuzi Dumo Nandu ‘Kolina’ kuvunja pambano hilo baada ya mashabiki kuingia uwanjani kufanya fujo.

Mchezaji mwingine nyota wa Yanga aliyekuwepo na kucheza mechi hiyo ni Oscar Joshua, huku mchezaji wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ naye akiongoza jahazi hilo.

Mashabiki wa Galatasaray walipinga uamuzi uliotolewa na mwamuzi huyo aliyepinga bao la kusawazisha dakika 80 kwa kile alichoeleza kuwa lilikuwa bao la kuotea.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Amos Mgisa wa JKT Ruvu na Omary ‘Otega’ kutoka Simba B wakati Kisiga alisawazisha bao kwa upande wa Galatasaray bao lililokataliwa lilifungwa na Shengo Hamisi (Villa Squad).

Mechi hiyo ilitawaliwa na wachezaji mbalimbali wanaoshiriki Ligi Kuu wakiwemo Sami Kessy, Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar) na Julius Mrope ambaye ni mchezaji huru hao waliichezea Galatasaray.

Mdau wa soka aliyekuwepo uwanjani hapo anayefuatilia mwenendo wa ligi hiyo (jina tunalo) alisema: “Twite na Ngassa walikuwa benchi, nafikiri Ngassa hajacheza kwa sababu anaumwa, Twite labda angeingia lakini kutokana na vurugu zilizojitokeza mpira ukavunjika, itapangwa tarehe nyingine ya kurudia mechi hiyo,” alisema Ngamba.

Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alipoulizwa kuhusu hilo alisema kuwa watafanya uchunguzi na wakibainika kukutwa na kosa basi hatua dhidi yao zitachukuliwa.

“Bado hatujapata taarifa hizo, lakini nitafuatilia na ikibainika basi kesho (leo Alhamisi) tutalijadili na wenzangu kujua tunachukua hatua gani, ila hairuhusiwi mtu mwenye mkataba sehemu nyingine kufanya kazi kwingine na wanafahamu hilo,” alisema Njovu.

Kwa upande wa Azam, mwenyekiti wao, Said Mohamed, alisema: “Hutumkatazi mchezaji kuchezea timu anayoipenda mtaani kwao, lakini anapaswa kutoa taarifa ili apewe ruhusa kwani anaweza kuumia, sisi huwa tunawahudumia, je akiumia huko nani atamhudumia?

“Tutalifuatilia hilo na litapelekwa kamati ya nidhamu ili kuchukua hatua ila leo (jana) wachezaji wote wameenda Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi,” alisema.