Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nestory Irankunda mambo magumu

IRANKUNDA Pict

Muktasari:

  • Winga huyo ambaye kwa sasa ana uraia wa Australia, alijiunga na mabingwa hao wa zamani wa Ujerumani akitokea Adelaide United ya Ujerumani aliyoitumikia kwenye timu za vijana za U-19, 21.

MAMBO yanaoneka kuwa magumu kwa winga mwenye asili ya Tanzania, Nestory Irankunda anayekipiga Grasshopper Club Zurich ya Uswisi kwa mkopo akitokea Bayern Munich.

Winga huyo ambaye kwa sasa ana uraia wa Australia, alijiunga na mabingwa hao wa zamani wa Ujerumani akitokea Adelaide United ya Ujerumani aliyoitumikia kwenye timu za vijana za U-19, 21.

Irankunda alishindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Bayern kilichosheheni nyota wakali kama Harry Kane na hivyo alitolewa kwa mkopo kwenda Uswisi.

Grasshopper ambako hadi sasa amecheza mechi 13 hajafunga bao lakini ametoa assisti tatu kwenye mechi 13 alizocheza.

Bayern ilimtoa kwa mkopo nyota huyo ili akapate uzoefu na akionyesha makali arejeshwe kikosini hapo.

Hata hivyo, kwa hali ilivyo ni wazi mambo yanaweza kwenda kombo kutokana na muendelezo mbaya wa kutotikisa nyavu kwenye mechi 13 alizocheza.

Tetesi zinaeleza Bayern wanataka kusajili mawinga wengine na kwa mwenendo huo huenda kinda huyo akakosa nafasi ya kurejeshwa kabisa kikosini hapo.