Ni Phantom, Igoma au Copco tu Mwanza

Muktasari:
- Phantom FC, Igoma Heroes na Copco Veterani kila moja ina nafasi ya kubeba ndoo kulingana na matokeo yao katika mechi za kufungia msimu zitakazopigwa Uwanja wa Nyamagana.
KITENDAWILI cha timu ipi itakayotwaa ubingwa wa Mkoa wa Mwanza kinatarajiwa kutenguliwa leo Jumanne kwa timu tatu kati tisa moja wapo kutangazwa kuwa wafalme wa Ligi Daraja la Tatu mkoani humo.
Phantom FC, Igoma Heroes na Copco Veterani kila moja ina nafasi ya kubeba ndoo kulingana na matokeo yao katika mechi za kufungia msimu zitakazopigwa Uwanja wa Nyamagana.
Phantom FC inaongoza ikiwa na pointi 18, ikifuatiwa na Igoma FC yenye alama 16 huku Copco Veterani yenyewe ikiwa na pointi 15.
Hata hivyo Copco itakuwa na kibarua kigumu watakapovaana na vinara Phantom kwani sare inaweza kuwafanya wapishane na ubingwa na kuwapa nafasi wapinzani wao kuweka rekodi jijini hapa.