Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okello awekewa medali ya ubingwa

OKELLO Pict


NYOTA wa Yanga, Allan Okello atakabidhiwa medali ya ubingwa wa Ligi Kuu Uganda msimu huu baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha Vipers kilichoanza safari ya kutwaa taji hilo kabla ya kutua Jangwani wakati wa dirisha dogo la usajili.


Okello alijiunga na Yanga Januari 2026 akitokea Vipers, hatua iliyofunga ukurasa mwingine wa ushindani nje ya mipaka ya Uganda.


Kabla ya kuondoka Uganda, kiungo huyo alikuwa ameifungia Vipers mabao matatu, akiwa bado sehemu muhimu ya kikosi kilichokuwa kikiwania ubingwa wa ligi nchini humo.

OKE 01

Mchango wake Vipers haukuishia hapo, kwani msimu uliopita alikuwa mmoja wa nyota walioiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na Uganda Cup.

Okello pia alimaliza msimu wa 2024-2025 kama mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda akiwa na mabao 19, jambo lililoonyesha ubora wake wa kipekee akiwa kiungo mshambuliaji.

Kwa ujumla, akiwa Vipers nyota huyo alihusika kwenye mabao 24 na asisti 13 katika mechi 58 za ligi, akijijengea jina kubwa kabla ya Rais wa Yanga, Hersi Said kumfuata na kukamilisha dili la kutua Jangwani.

OKE 02

Takwimu hizo zilimfanya kuwa mmoja wa viungo hatari zaidi waliowahi kucheza Ligi ya Uganda kwa miaka ya hivi karibuni, kutokana na uwezo wake wa kufunga na kutoa asisti.

Hata hivyo, licha ya kutua Yanga katikati ya msimu, Okello ameonyesha kuwa moto wa kuotea mbali kufuatia kufunga mabao tisa na kutoa asisti saba kabla ya mechi ya jana Jumatatu dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam.

OKE 03

Kama ataisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, basi atakuwa amebeba medali mbili za ligi tofauti ndani ya msimu mmoja huku akionyesha kiwango bora. Vipers imetwaa ubingwa baada ya kumaliza msimu ikiwa na pointi 67 zilizotokana na kushinda mechi 19, sare 10 na kupoteza moja.