Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida BS, Kagera Sugar kupindua meza?

SINGIDA Pict

Muktasari:

  • Timu zilizofuzu ni Singida Black Stars iliyoitoa KMC FC kwa kuichapa bao 1-0, maafande wa JKT Tanzania wakaichapa Mbeya Kwanza mabao 3-0, huku Kagera Sugar ikiitoa Tabora United kwa penalti 5-4, baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

MICHUANO ya Kombe la Shirikisho (FA), imefikia patamu, huku tukishuhudia timu nane zikitinga hatua ya robo fainali kwa ajili ya kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Katika timu nane zilizofuzu hatua ya robo fainali, rekodi zinaonyesha hakuna iliyochukua ubingwa zaidi ya Yanga na Simba kuanzia michuano hiyo iliporejea msimu wa 2015-2016, baada ya kutofanyika kwa kipindi cha miaka 13, tangu mwaka 2002, huku mtihani ukibaki kwa zingine kupindua utawala huo ikiwemo Singida Black Stars.

Timu zilizofuzu ni Singida Black Stars iliyoitoa KMC FC kwa kuichapa bao 1-0, maafande wa JKT Tanzania wakaichapa Mbeya Kwanza mabao 3-0, huku Kagera Sugar ikiitoa Tabora United kwa penalti 5-4, baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Zingine ni Simba iliyoifunga Bigman FC mabao 2-1, Yanga ikiitandika Songea United 2-0, wakati Pamba Jiji ilifuzu hatua hiyo pia baada ya kuwafunga ‘Wazee wa Mapigo na Mwendo’ Mashujaa FC 1-0, huku Mbeya City ikiichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1.

‘Chama la Wana’, Stand United ikafuzu hatua hiyo baada ya kuwafunga Mabingwa wa Mkoa wa Katavi, Giraffe Academy mabao 3-1, hivyo kuhitimisha timu mbili tu za Championship zilizofuzu robo fainali, huku zile za Ligi Kuu Bara zikiwa sita.

Akizungumzia kitendo cha kufuzu robo fainali, Kocha wa Pamba, Fredy Felix ‘Minziro’, alisema mojawapo pia ya malengo yao makubwa ni kufanya vizuri katika michuano hiyo, huku akiwapongeza wachezaji kwa kuonyesha nidhamu kubwa wakiwa ugenini.

Tangu michuano hiyo iliporejea msimu wa 2015-2016, Yanga ndio timu inayoongoza kwa kuchukua ubingwa huo mara nyingi zaidi, baada ya kufanya hivyo mara nne, ikifuatiwa na wapinzani wao wakubwa Simba, waliolichukua taji hilo mara tatu tu.

Timu nyingine zilizochukua ubingwa huo tangu kipindi hicho mbali na Yanga na Simba, ni Mtibwa Sugar na Azam FC ambazo zote tayari zimetolewa, jambo linalosubiriwa kuona ni ipi kati ya zilizobaki inayoweza kupindua ufalme kwa miamba hiyo.