Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Srelio yastukia jambo, JKT ikijibu mapigo

SCERIO Pict

Muktasari:

  • Kocha wa timu hiyo, Miyasi Nyamoko amesema klabu yake imejipanga kushusha nyota wake kabla ya ligi hiyo kuanza Mei 10, mwaka huu ili ianze mapema kufanya maandalizi ya mwisho mwisho ikiamini kwamba kwa sasa wanaendelea kujifua huko waliko.

BAADA ya uongozi wa Chama cha Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD) kutangaza kwamba ligi mkoani humo (BDL) itachezwa katika mzunguko mmoja timu ya Srelio imeshtukia jambo na sasa imepanga kuwashusha nyota wake mapema jijini humo ili kujiandaa kwa ajili ya mashindano hayo.

Kocha wa timu hiyo, Miyasi Nyamoko amesema klabu yake imejipanga kushusha nyota wake kabla ya ligi hiyo kuanza Mei 10, mwaka huu ili ianze mapema kufanya maandalizi ya mwisho mwisho ikiamini kwamba kwa sasa wanaendelea kujifua huko waliko.

Nyamoko amesema hayo ni baada ya uongozi wa chama hicho na viongozi wa klabu kukubaliana ligi hiyo ichezwe katika mzunguko mmoja badala ya miwili.

Kwa mujibu wa Nyamoko, timu yake iliyozoeleka kuanza vibaya katika mzunguko wa kwanza ilikuwa ikifanya hivyo kutokana  na kutokuwepo kwa nyota wake mapema miongoni mwao wanaoishi mikoani na nje ya nchi.

“Kwa sasa tunajipanga kuwaleta nyota hao mapema kwa lengo la kutoa ushindani mkubwa katika BDL mwaka huu," alisema kocha huyo akiwataja miongoni mwao kuwa ni Spocian Ngoma na Joseph Kamamba wanaoishi Zambia, Chary Kesseng (Cameroun) na Zadock Emanuel anayetokea Kenya.

Ubora wa Srelio katika ligi ya kikapu mwaka jana kwenye mzunguko wa pili uliiwezesha kuzifunga Dar City kwa pointi 78-75, Savio 75-69 na Vijana maarufu City Bulls kwa pointi 69-65.

Baada ya hapo timu hiyo ilitinga robo fainali kisha ikatolewa na JKT katika michezo 3-1. Timu 32 zinatarajiwa kushiriki katika ligi ya kikapu mkoani humo mwaka huu, ambapo kati ya hizo 16 ni za wanaume na 16 wanawake.

SCE 01

JKT YAJIBU

Katika hatua nyingine JKT imefanya kweli baada ya kusajili nyota watatu wazawa kwa mpigo ambao ni Alfan Mustafa iliyemdaka kutoka Vijana, Baraka Sabibi (UDSM Outsiders) na Jordan Manang aliyetokea Mchenga Star.

Mbali ya kuwasajili wachezaji hao pia imempandisha Adam Lutungo aliyekuwa akichezea kikosi cha pili cha Mgulani JKT.

Usajili wa wachezaji hao ni kama jibu baada wachezaji wake Jonas Mushi na Felix Luhamba kutimkia Stein Warriors.

Mustafa anayecheza kama namba moja (point guard), katika BDL alishika nafasi ya tisa kwa kutoa asisti 82 msimu uliopita, huku Jordan anayecheza namba nne (power forward) ni mchezaji mwenye nguvu zaidi akiwa na uwezo wa kupambana katika kufunga karibu na goli pamoja na kudaka mipira (rebound) ambapo alishika nafasi ya sita kwa udakaji wa mipira ya rebound 209.

Naye Sabibi anayecheza namba mbili (shooting guard) sifa aliyo nayo ni kwamba ana uwezo wa kumsaidia mchezaji anayecheza nafasi ya point guard na katika ufungaji ni fundi wa kufunga katika eneo la mtupo mmoja (three point).

Akizungumza na Mwanaspoti Manang, alilimbia Mwanasposti kuwa amejiunga na JKT kwa lengo la kuongeza ubora katika uchezaji wake. 

“Kujiunga JKT naamini nitashirikiana na wachezaji wenzangu vizuri kutetea ubingwa mwaka huu,” alisema Manang.

SCE 02

TIMU ZA WANAWAKE ZISHUKE DARAJA

Akizungumza kuelekea kuanza kwa ligi hiyo kocha wa timu ya vijana wilayani Ilala, Ally Said ameshauri timu zitakazoshika nafasi tatu za chini katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam upande wa wanawake (WBDL), mwaka huu nazo zishuke daraja kama zilivyo za wanaume. 

Saidi anayefundisha vijana wa umri wa miaka 14, alisema kufanya hivyo kutafanya timu ziongeze jitihada katika kupambana kuwania ubingwa na kujihami ili zisishuke.

“Timu za wanawake zimekuwa zikicheza bora zimalize ligi kutokana na kujiamini kwamba hazitaguswa,” alisema Said na kuongeza kuwa kwa miaka minne mwamko mwa timu hizo umeongezeka huku mpya zikianzishwa.

“Ushauri wangu kwa uongozi wa BDL timu zitakazoomba kucheza ligi zicheze na timu zitakazoshuka daraja kama zilivyo kwa timu za wanaume zishuke.”

Kwa mujibu wa Said haiwezekani timu zinaomba kucheza ligi kubwa na wachezaji, lakini hazipimwi ipasavyo ili zisizostahili zishuke daraja.