Stars yabadili gari kukwepa figisu

Muktasari:
Lakini leo wameamua kukodi Bus lingine kubwa huku lile ambalo walipewa wamemua kulipeleka kwa wanafunzi ambao watajitokeza katika kushangilia timu hiyo na kufanya Stars kubadili gari mara tatu tangu wawasili nchini hapa.
VIONGOZI walioambatana na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wamefanya mabadiliko ya usafiri wanaotumia na kuchukua gari lingine.
Stars ambayo iliwasili nchini hapa Jumanne ilifika na kupokelewa na gari lingine lakini baada ya kwenda hotelini walibadilisha.
Jana Alhamis, Stars walikuwa wakitumia basi lingine lenye rangi nyekundu kwaajili ya kwenda mazoezini na mizunguko mingine.
Leo Ijumaa, wameamua kukodi gari lingine kubwa huku lile ambalo walipewa wamewapelekea wanafunzi ambao watajitokeza kuishangilia Stars watakapocheza na Sudan usiku wa leo, saa 2.
Katika mazingira ya hoteli yao waliyofikia hakuna shamrashamra yoyote bali kumekuwepo na utulivu wa hali ya juu huku kukiwa na viongozi wakiwa nao wametulia wakisubiri muda.